Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - JK aitisha kikao cha Ulinzi, Usalama

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MILIPUKO ya mabomu iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika ghala la kuhifadhia silaha katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), huko Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, imevuruga shughuli za Bunge na kumlazimisha  Rais Jakaya Kikwete, kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Taarifa kuhusu kikao hicho cha dharura, zilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipokuwa akitoa tamko rasmi ya serikali juu ya  tukio hilo, lililosababisha makumi ya raia kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.


Waziri Pinda aliliambia Bunge kuwa kufuatia tukio hilo, Rais Kikwete ameitisha kikao cha dharura wa Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama, ili kujadili mambo kadhaa, likiwamo la kuundwa kwa mabaraza maalumu ya kuchunguza tukio hilo.

"Kwanza nianze kwa taarifa fupi ya tukio la jana (juzi) usiku, ili Bunge lako lijue maendeleo ya tukio hilo. Jana (juzi) tarehe 16 Februari majira ya saa 2:20 usiku ulisikika mlipuko katika moja ya maghala ya kuhifadhia silaha ghala namba tano, linalohifadhi silaha mchanganyiko."

Alisema kufuatia mlipuko huo, maghala mengine yalianza kulipuka kwa kishindo kikubwa."Kutokana na mlipuko huo maghala mengine yalianza kulipuka na kishindo kilikuwa kikubwa sana,"alisema Pinda.

Kwa mujibu wa waziri mkuu, hali iliendelea na lipofikia saa 11 alfajiri maghala 22 yalikuwa yameshalipuka na kubakiwa na ghala moja namba 23.

Alisema baadaye, hali ilitulia kidogo na hivyo kutoa mwanya kwa viongozi wa jeshi kuingia katika eneo la tukio, ili hali halisi kuhusu kilichotokea.

Kwa mujibu wa Pinda mabweni mawili ya askari wa JWTZ yaliteketea katika tukio hilo.Hali kadhalika magari 22 yaliyokuwa katika eneo hilo na nyumba mbili za jirani.

Alisema moja ya mabomu hayo, lilioangukia katika moja ya shule za sekondari, iliyoko jirani na eneo hilo na kuharibu chumba cha darasa.Alisema tayari Rais alikwishaarifiwa kuhusu tukio hilo na kwamba  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zote za mkoa huo, zilikuwa zimeanza kazi ya kushughulikia tukio hilo.

Pinda aliwataja mawaziri waliokwenda Dar es Salaam kushiriki katika kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama kuwa ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussen Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Nahodha na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo.

Kuhusu hatua zilizochukuliwa na jeshi baada ya milipuko kutulia, waziri mkuu alisema ni pamoja na kutathmini kiwango cha uharibifu.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watu waliokufa hadi jana asubuhi ilikuwa 17, lakini kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuongezeka.
Tags:

0 comments

Post a Comment