Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Chadema wapokelewa Butiama na Kuungwa mkono na Familia nzima ya Mwl. Nyerere

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere

MJANE wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, jana aliwaombea dua njema kwa Mungu, viongozi wakuu wa Chadema huku mtoto wake, Madaraka Nyerere, akikitabiria chama hicho kupata ushindi wa kura milioni sita dhidi ya kura milioni nne za CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 .

Hatua hiyo inakuja wakati viongozi wa chama hicho cha upinzani, wakiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuendesha maandamano ya kuishinikiza serikali, isilipe tuzo ya Sh94 bilioni kwa Kampuni wa Dowans.

Tuzo hiyo imetolewa na Mahakama ya Kimatafa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba kati yake na Dowans.

Maandamano ya Chadema katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, yamekuwa yakiungwa mkono na maelefu ya wananchi.

Jana maandamano hayo yalifanyika katika Kijijni cha Butiama, Musoma Vijijini alikozaliwa na kuzikwa mwasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.Viongozi wa chama hicho na baadhi ya wananchi, walikwenda kwenye kaburi la kiongozi huyo, ili kuomba dunia.

Akizungumza mbele ya kaburi hilo, Mama Maria aliomba akisema "mtumishi wa Mungu, tazama hawa viongozi wanaokuja mbele yako, wanafanya kazi, tunakuomba kila mmoja wao umwezeshe kutambua kuwa yeye ni mtumishi wa watu tu."


Hata hivyo, jukumu la kuzungumza alipewa Madaraka ambaye alisema aliposikia habari kuhusu maandamano, hakuelewa vizuri, lakini sasa ametambua na kuamini kuwa hilo ni jambo jema.

Madaraka alisema kwa muda mrefu amekuwa akikitambua chama tawala na kwamba alikuwa hawajui Makongoro na Mbowe akimaanisha kuwa taifa halikuwa na ubaguzi wa dini wala ukabila.Alisema hata hiyo sasa ameanza kutambua na kuona tofauti.

"Kazi ya upinzani ni kusaka kura. Nilisikia katika uchaguzi uliopita kuwa watu walipiga kura na wengine hawakupiga kura. Sasa nadhahi mwaka 2015 watakaopiga kura watakuwa milioni 12 na CCM watapata kura milioni sita lakini, Chadema wao watapata kura milioni sita. Hizi nyingine milioni mbili zitakuwa za watu ambao hawatapiga kura," alisema Madaraka.

Madaraka pia ni mume wa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema, Leticia Nyerere.

Kabla ya kuchaguliwa mbunge wa viti maalumu, Leticia aligombea ubunge katika Jimbo la Kwimba, lakini alibagwa Shanif Mansoor wa CCM.

Mbali na Leticia Nyerere, Chadema ina mbunge mwingine kutoka katika familia ya Baba wa Taifa, anayejulikana kwa jina la Vicent Nyerere. Vicent ni mbunge wa kuchaguliwa katika Jimbo la Musoma Mjini.

Madaraka alisema kwa sasa hana shaka na Chadema kwa sababu chama kinakubalika kwa wananchi na kwamba hiyo inatokana na jinsi viongozi wanavyojipanga.


Alisema kujipanga huko ni pamoja na kupita mikoani wakitetea wananchi na kunadi sera.

Madaraka alisema wakati fulani hakuelewa mantiki ya wabunge wa Chadema, kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, lakini sasa anajua.

"Lengo lenu ni zuri, unaweza kuwa na lengo zuri sana lakini likapotoshwa kwa makusudi. Kwa hiyo mkipita kuwapambanulia wananchi, wataelewa tu," alisema Madaraka.

Katika Kijiji cha Butiama, wabunge hao na viongozi wa Chadema, walikaribishwa na mtoto mwingine wa hayati baba wa taifa Makongoro Nyerere, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara.

Baada ya kupokewa na Madaraka Nyerere, walisalimiana na Mama Maria Nyerere na baadaye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimshukuru kwa kuwakaribisha Butiama.

"Tunakutakia mema, tunakuomba utuombea, tunaomba utuunge mkono pale panapotakiwa, taifa letu bado linaitegemea familia yenu," aliomba dua Mbowe.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa sala katika kaburi la Baba wa Taifa, Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk Willbroad Slaa, alisema kwa sasa kanisa liko katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu.

Dk Slaa alitilia mkazo mchakato huo akiwataka  Watanzania kuombea suala hilo ili likamilishwe kwa wakati uliopangwa.

Tags:

0 comments

Post a Comment