Hawa Ghasia (aliyesimama) |
Tayari, Ghasia kwenye Bunge la Tisa aliwahi kuonya watumishi wa umma wanaovujisha nyaraka za siri za serikali, kauli ambayo ilionekana kwa wakati huo kuchukizwa na mabomu aliyokuwa akiyarusha Dk Willibrod Slaa, akiwa Mbunge wa Karatu.
Ghasia alirejea kilio hicho juzi akifafanua mbele ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, na kuweka bayana kuwa serikali inaendelea kupambana na tatizo hilo.
Hata hivyo, akichangia hoja hiyo Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, alihoji jinsi uvujaji huo unavyoendelea na wahusika wakiwamo wabunge hasichukuliwi hatua.
Mtemvu alifafanua kwamba wabunge hawako juu ya sheria, hivyo kama wanakutwa na nyaraka hizo za siri za serikali, ni vema wangechukuliwa hatua za kisheria.
“Waziri umeelezea hili la kuvuja kwa nyaraka za siri za serikali. Mimi nasema kama nyaraka zinavuja na wahusika wanajulikana hata kama ni sisi wabunge sheria ichukue mkondo wake,” alisisitiza Mtemvu.
Mtemvu alisema nyaraka za siri wakati mwingine zinasambaa hadi mitaani na kutumika kufungia maandazi.
Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, akichangia taarifa hiyo alisema kitendo cha kutokea matatizo ya mikataba kama Richmond kinaonyesha kuna tatizo kwa watumishi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Blandes alihoji uwezo wa watumishi wa ofisi ya AG na kusisitiza: “Serikali lazima iwaendeleze vijana elimu...kwa sababu haitoshi tu kumchukua mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam halafu akae pale aingie mikataba mikubwa ya kimataifa.”
“...hawa lazima wapewe elimu zaidi ili waweze kukabiliana na mahitaji makubwa ya ushindani wa kitaaluma katika kuandaa mikataba mbalimbali mikubwa ya kimataifa.”
Kuhusu watumishi hewa, Blandes alishangaa kuona karne hii ya sayansi na teknoloji serikali inaendelee kulia na watumishi hewa wakati kuna mfumo imara wa kuhifadhi taarifa kwa kompyuta.
Kuhusu ongezeko la mishahara ya watumishi, mbunge huyo aliweka bayana kwamba kwa kuangalia ukali wa maisha ikiwamo mfumko wa bei ya vitu, serikali imekuwa ikihadaa watumishi katika kile inachokiita nyongeza ya mshahara.
0 comments