Mazungumzo yanaendelea Arusha, makao makuu ya Jumuia ya Afrika mashariki nchini Tanzania, juu ya uwezekano wa kuwa na sarafu moja kwa eneo hilo la Afrika.
Maafisa wanaowakilisha Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, wanakutana kwa siku nne kujadili jinsi sarafu hiyo ya pamoja namna itakavyoafikiwa.
Hii na awamu ya tatu ya kujaribu kuziunganisha nchi za Afrika kwa lengo la kurahisisha na kupunguza gharama za biashara.
Lakini wadadisi wamesema mradi huo utaleta wasiwasi katika eneo hilo kusipozingatiwa kuwepo kwa umoja wa kisisasa kwanza.
0 comments