Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Akiri Katiba ya Z’bar, Muungano kugongana

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari, amekiri katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinagongana kiuandishi.

Alisema kutokana na hali hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya kwa lengo la kuondoa utata unaojitokeza, hasa kwa kuanisha histoia ya nchi mbili zilizounda Muungano huo.

Alikuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Issa Jecha Simai, aliyetaka kujua katiba ambayo inatakiwa kufuatwa na wananchi kutokana na zilizopo kugongana kiuandishi.

Waziri Abubakar alikiri kifungu namba 2(a) cha katiba ya Zanzibar kinampa uwezo Rais wa Zanzibar kugawa Zanzibar kwenye mikoa, wilaya na maeneo mengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Pia, ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri inampa uwezo Rais wa Muungano kuigawa Jamhuri ya Muungano kwenye mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu, lakini kwa Zanzibar analazimika kushauriana na Rais wa Zanzibar.

“Ni kweli katiba hizi mbili zinazogongana kiuandishi, hivyo katiba ya Jamhuri inapaswa kuangaliwa upya ili kuondoa utata huo, hasa kuainisha historia ya nchi hizi mbili na kuainisha mamlaka na majukumu ya serikali hizi mbili kulingana na mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Alisema upande wa mambo ya Muungano, katiba inayopaswa kufuatwa ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mambo yasiyohusu Muungano kwa Zanzibar, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Zanzibar ya mwaka 1984  kama ilivyorekebishwa kwa nyakati mbalimbali.

Hata hivyo, Waziri Abubakar alisema marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yamezingatia zaidi maamuzi ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa serikali, ambao utendaji wake utafanywa kwa utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini kwa lengo la kufikia demokrasia.
Tags:

0 comments

Post a Comment