Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Chadema: Serikali itoe tamko vurugu Arusha

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KATIBU wa Kambi ya Upinzani Bungeni,John Mnyika amelitaka  Jeshi la Polisi,  Waziri Mkuu, Ofisi ya Bunge na chama tawala cha CCM kutoa tamko kuhusu kitendo cha kupigwa kwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Lema alipigwa vibaya na askari wa Jeshi la Polisi wakati alipokwenda kwenye mkutano wa madiwani kupinga uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha, akidai kuwa mkutano huo wa uchaguzi uliitishwa kinyemela kwa kushirikisha madiwani wa CCM na TLP tu.
Katika mkutano huo wa uchaguzi, diwani wa CCM wa Kata ya Olorien, Gaudence Lyimo alichaguliwa kuwa meya na nafasi ya naibu meya kwenda kwa diwani wa Kata ya Sokoni (TLP), Michael Kivuyo.
Mnyika, ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alisema ameshangazwa na tukio hilo kwa kuwa polisi wameamua kuwapiga wananchi ambao hawakufanya fujo wala kuwa na silaha ya aina yoyote.

“Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema  kutoa tamko  kali dhidi ya askari polisi waliohusika kupiga wananchi, akiwemo mbunge wa Chadema,” alisema Mnyika.

“Picha zipo wazi na askari waliohusika katika tukio hili na wanaonekana wazi, kwa hiyo IGP pia achukue hatua kali kwa askari waliohusika. Hakuna sheria inayomtaka polisi kupiga raia ambao hawakufanya fujo wala kuwa na silaha za aina yoyote.”
Alisema pia anamtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa tamko la kulaani kitendo hicho kwa kuwa limetokea katika uchaguzi wa Umeya ambao kimsingi upo chini ya Wizara ya Tamisemi.

“Ili uingie bungeni kama si mbunge kuna kanuni na taratibu zake, sasa iweje leo polisi waingie katika mkutano wa baraza la madiwani tena wakiwa na silaha,” alihoji Mnyika.

Mnyika alifika mbali na kusema kuwa pia Ofisi za Bunge zinatakiwa kulitolea tamko tukio hilo kwa kuwa linamhusu mbunge ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake na kwamba kitendo cha kupigwa ni sawa na kuingilia maslahi ya mbunge.
“Chadema nao wanatakiwa kulitolea tamko tukio hili, nasema hivi kwa kuwa Chadema iliwahi kusema kuwa vyombo vya dola ndio vitakavyosababisha umwagaji damu na jambo hilo limedhihirika wazi,” alisema Mnyika.
“Hata CCM nao wanatakiwa kusema kitu kuhusiana na suala hili kwa kuwa ulikuwa uchaguzi unaokihusisha chama hicho.”
Lakini imesema itakuwa vigumu kutoa tamko au kulizungumzia suala hilo kwa kuwa lina mwelekeo wa kisheria.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili na kueleza kuwa hata hivyo serikali haina taarifa ya kupigwa kwa mbunge huyo.

“Siwezi kuzungumza lolote kuhusu tukio la kupigwa kwa Mbunge Lema, kwa kuwa bado sijapata taarifa rasmi ya tukio hilo. Nimelisikia kupitia vyombo vya habari,’’ alisema Lukuvi.
Wakati huohuo, hali ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema inaendelea vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Mbunge huyo aliliambia gazeti hili jana kuwa aliruhusiwa kutoka hospitalini juzi saa 1:30 usiku baada ya kuona hali yake inaendelea vizuri.

Lema alisema baada ya kufanyiwa vipimo mbalimbali madaktari hao walibaini kuwa alipatwa mshituko wa shinikizo la damu kutokana na kipigo hicho cha polisi.
“Ni ajabu sana polisi kupiga raia kama mimi hovyo; nimeumia sana na nimedhalilishwa lakini ninajiandaa kuwachukulia hatua kwa kuwa nawajua kwa sura na nitaendelea kupambana kudai haki yangu hadi kieleweke,” alisema mbunge huyo
Diwani wa Kata ya Elerai (Chadema), John Bayo alisema leo wanatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi kupinga uchaguzi huo kutokana na baadhi ya kanuni kutofuatwa.

Comments 

0#15 OSCAR 2010-12-20 15:32
Pole sana Mh. Lema Mungu atakusaidia. Mh. Lukuvi aone aibu kutamka hajapata taarifa, nadhani hajui wajibu wake kama waziri ni upi. Hii ndio aina ya viongozi tulionao bado wana mawazo ya kikoloni, wanataka wananchi wawatumikie wao badala ya wao kuwatumikia wananchi. Hivi inaingia akilini waziri unakaa ofisini unasubiri uletewe taarifa wakati ndani ya nchi yako kuna vurugu, unategemea taarifa akuletee nani huyo aliyesababisha vurugu? Nawaasa viongozi wetu hii sio karne ya kukaa ofisini nendeni mkawatumikie wananchi bila upendeleo wowote. Fanyeni maamuzi kwa kumwogpa Mungu, haya yote yana mwisho wake.
Quote
0#14 Mjuba 2010-12-20 15:30
Hii ni kali, sisis ambao tuko Arusha tulishuhudia hiki kitendo na si kizuri kwa jamii, nadhani kamanda Andengenye anatafuta namna ya kutoka yaani atoke vipi, sasa tunamtaadhalish a afuate sheria na si kuwasikiliza wakubwa wake wanachomuamuru kukifanya kwani nayeye ana akili timamu anaweza kuyapima maamuzi ya wakubwa kwanza kabla ya kuyatekeleza kama alivyokuwa Kamanda Basilio, cha kuangalia Kamanda Materu ni kuwa hii ni Arusha na uzuri zaidi ulishawahi kuishi hapa mji huu ni mdogo na kwa kweli watu wake ni wastaarabu, hawataki shari, wanapendana hivyo usije ukaweka uadui kati ya raia na polisi je polisi jamii itafanikiwa? Mbunge amechaguliwa na wananchi na anahadhi kubwa kuliko hata ya viongozi wa kuteuliwa na si mtu kama Mbunge ambaye umma ndio umempa ridhaa ya kukaa ofisini.
Hivyo tunaomba nidhamu ndani ya vijana wako hapa Arusha. Mungu Ibariki Tanzania.
Quote
0#13 Muddy 2010-12-20 14:30
Hii ndo TANZANIA nchi yenye amani ya unafiki hivi hawa polisi kweli wanafundishwa sheria na wajibu wao kweli? Maana kila kukicha utasikia haya mara yale kwa hali hii MAANDELEO HAYAJI NG'O. POLE SANA GODBLESS LEMA.
Quote
0#12 KATIBA Mpya 2010-12-20 14:17
Police TZ awana aibu!


Wanadhani kuvaa magwanda ndio sheria iwe chini yao,kwamba wanaweza kunyanyasa wananchi kama enzi ya ukandamizaji wa haki za binadamu za mfumo wa chama kimoja cha CCM na siasa zao za alinacha za Ujamaa na Kujitegemea?!!!!


KATIBA Mpya inakija, na haki za binadamu watazielewa vzr, mfumo wa mabavu umefika kikomo.


Viongozi wa CCM na police , The Hague itakuwa mwisho wenu. mtanyooka kwa sheria sio kujichukulia madaraka mikononi.
Quote
0#11 elibariki Yerald 2010-12-20 14:03
CHAKACHUA MATOKEO WANATAKA KUIPELEKA NCHI HII,TUIKOTAKA TUFIKE,SEHEMU ZOTE AMBAZO CHADEMA WAMEONEKANA KWENDA KUSHINDA UCHAGUZI WAMECHAKACHUA UCHAGUZI NA KUTUMIA DOLA WANATAKA SASA TUSHIKE BUNDUKI????? NILISHASEMA IKO HATARI KUBWA INAYOKUJA NA WAHAMASISHAJI WA HAYO NI CHAMA CHA MAJAMBAZI,,HIVI MBONA MNATAKA KUTUFANYA WATANZANI AHATUA AKILI!!!!!1
HIVI MNAFIKIRI HATUPO KUMWAGAA DAMU KAMA IVORY COAST,KENYA,ZIM BABWE NA KWINGINEKO NI BORA KUFA NIKIWA NAPIGANIA HAKI YA WALIO WENGI KULIKO KUWAACHA WATU WAKINYANYASWA NA VIONGOZI UCHWARA! MAANA DAMU IKIMWAGIKA NDIPO WATU WATAJIFUNZA NDIO MAANA WAASISI WETU WALIKATAA UKOLONI ILI NCHI YETU IKOMBOLEWE, NA SASA TUPO NA WAKOLONI WEUSI,IPO SIKU ITATULAZIMU KUFANYA HIVYO MAANA TABIA YA BINADAMU IKIFIKA KIPINDI AMECHOKA KUNYANYASWA HUWA TAYARI KWA LOLOTE HATUPO TAYARI KWA HILO
LAKINI MAZINGIRA NA NYAKATI YANAWEZA KUSABABISHA HAYO KUTOKEA,MAAN KUNA UTUIVU KATIKA NCHI YETU,AMANI HAKUNA,WATU WANANYANYASWA,H AWAPATI MAJI SAFI,,WANABAMBI KIWA KESI,HHAWAPATI ELIMU KWASABABU NI MASKINI ,WATOTO WACHANGA NA AKINA MAMA WANAFARIKI KWA SABABU HAKUNA HOSPITALI NA ZAHANATI (KUMBUKA YULE MAMA ALIYEJIFUNGUA WATOTO 5 NA SASA NI WAILITU WANAISHI HUKO SHINYANGA) WATU WACHACHE WANATAFUNA RASILIMALI ZA NCHI YETU
TUMECHOKA KUONEWAAA! KUNYANYASWA, NA KUKANDAMIZWAAAA MUDA SIO MREFU MTAONA KUWA WATANZANIA WANA AKILI AU NI MAMBUMBU.
Quote
+1#10 Mkaa mbichi 2010-12-20 12:48
Nadhani ni wakati mzuri wa kuanzisha mapambano ya kweli. Where is my g*n?
Quote
+1#9 mdanganyika 2010-12-20 12:26
CCM mjifunze kukubali matokeo vinginevyo patachimbika kama Somalia hapa.
Quote
0#8 Kezilahabi 2010-12-20 12:24
CCM wanazidi kuipa CHADEMA umaarufu. Na kwa mara nyingine tena TLP wanathibitisha kuwa wao ni mamluki wa CCM.
Quote
+1#7 nguzu 2010-12-20 12:11
polisi daini masilahi yenu kama vile ongezeko la mishahara (mtabaki ninyi tu!) badala ya kuwapiga ndugu zenu (tena hawana silaha kama ishara ya kuvunja amani) kulinda maslahi ya kisiasa.


imeandikwa wazi hata katika katiba hii yenye viraka kuwa hamruhusiwi kufanya mambo ya siasa [Ibara 147 (3),(4)]


mtagombana bure na jamii inayowazunguka, kumbe tu baadhi yenu hamjui nini mnachokifanya!
Quote
+1#6 Kalonzo Musyoka 2010-12-20 11:21
Subira na uvumilivu wa watanzania unajiribiwa mno na serikali ya CCM na watendaji wake. Nadhani ni muhimu kwa serikali ya CCM kujua sasa tupo karibu kufikia ukingoi. Na kama ni vurugu za kisiasa au vita basi matendo yao haya ya kudhulimu haki zetu (mgombea huru, katiba mpya, tume huru vyombo vya dola vyenye kufuata sheria, Tukukuru inayowatumikia wananchi na sio mafisadi, spika wa wananchi sio mafisadi n.k.) ndio yatakayo anzisha vurugu. Nawasihi serikali ya CCM isiendelee kutujaribu kupita uvumilivu wetu
Quote
+1#5 GRACA ,MACHA 2010-12-20 10:28
Waziri mwenye dhamana ya suala hili mheshimiwa Lukuvi aone aibu kusema serikali haijapata taarifa amelisikia kwenye vyombo vya habari. Hakuwajibika kujua nini kinatokea kwa watu anaopaswa kuwajibika kwao na hivyo si vema na ni hatari. Lakini pia mazoea haya ni ya hatari kila siku jitihada zinafanywa kuwakasirisha wananchi, na mwajua kila mtu ana ukomo wa hasira. Kitakachotokea kama ndicho mnachotaka enyi mnaojiita 'serikali' msipowajibika hapa duniani kuna pengine mtakapowajibish wa tu, muwe na imani kwa Mungu au msiwe na imani kwake lazima dhamiri ziwasute na kuharibu familia zenu.


Polisi lindeni maslahi ya raia siyo masilahi ya 'serikali' maana hao waitwao serikali hawapo kama raia hawapo
Quote
+3#4 JOHN MAZANDA 2010-12-20 08:37
NI U[NENO BAYA] MKUBWA SANA KWA POLISI KUPIGA HOVYO RAIA WASIO NA HATIA.HIVI POLISI WA NCHII WANATAMBUA KWAMBA WAO SI WANASIASA JAMANI NA KWAMBA MABOSI WAO WANAWEZA BADILIKA WAKATI WOWOTE?KULIKUA NA HAJA GANI KUMPIGA NA KUMDHALILISHA MH. MBUNGE NDANI YA JIMBO LAKE NA KATIKA KIKAO KINACHOMHUSU?
Quote
+2#3 Jumanne 2010-12-20 08:27
Dawa ni kuifanya Tanzania kama Somalia,ni kujitoa mhanga na vituo vya Polisi tu. Polisi wanaonekana ni adui wa kubwa sana .Hawahiji kusamehewa hata kidogo. Dawa ni kulipua vituo vyao tu. Na popote unapomuona askari muone kama adui mkubwa.
Quote
+2#2 maharage 2010-12-20 08:08
VIONGOZI WOTE WA CCM NA SERIKALI YAO NI WABOVU NA WANAOLINDA MASLAHI ZAO NA FAMILIA ZAO BILA KUJALI WANANCHI WANACHOJALI NI KUTAWALA TU. SIASA SIO UGOMVI LAKINI WAO WANAAMRISHA POLISI KUTWANGA WATU PASIPO HATA NA KOSA. WAJIULIZE HIVI WATATAWALA MILELE, WATARUDI URAIANI NA HATA NDG ZAO TUKO NAO URAIANI NAONA WANAIGAWA TANZANIA KWA MASLAHI YAO
Quote
+3#1 Zinga 2010-12-20 07:38
Kama kanuni hazikufuatwa na uchaguzi ukafanyika huyo Mkurugenzi wa arusha kwanini hajafukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka ya kushindwa kutimiza wajibu wake na kuhujumu uchumi?. Kesi zimezidi na zitaligharimu sana taifa letu. Kesi za ubunge zinahitaji 2 bilioni na bado mnataka kufungua nyingine!!! Hawa wanaotutia hasara kwa kuendesha uchaguzi ovyo bila kufuata kanuni nashauri kwanza wafukuzwe kazi pili wafilisiwe na tatu wanyongwe!!
Quote

Tags:

0 comments

Post a Comment