Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Zitto afikia uamuzi jimbo atakalogombea

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameshafikia uamuzi wa jimbo ambalo atagombea kwenye uchaguzi mkuu na ameahidi kutangaza uamuzi wake rasmi mwanzoni mwa mwezi Juni.

Zitto alieleza kuwa amefikia hatua hiyo baada ya utafiti wake wa kisayansi pamoja na ushauri alioupata katika majimbo mawili kati ya matano aliyokuwa ameombwa agombee, kukamilika.

Jana Zitto aliiambia Mwananchi kuwa atautangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake wa hadhara ambao itakayofanyika Geita na Kigoma Kaskazini.

“Tayari nimeshafanya uamuzi wa jimbo nitakalogombea... uamuzi nitautangaza mwanzoni mwa mwezi Juni kwenye mikutano ya hadhara nitakoyafnya Kigoma na Geita,” alisema Zitto. Zitto alisema kuwa uamuzi huo atautoa mara baada ya kurejea kutoka nchini Ujerumani anakokwenda kikazi.

Machi 29 mwaka huu akizungumza katika Uwanja wa Magereza mjini Geita, Zitto alisema kuwa matokeo ya utafiti wake yalimfanya apunguze majimbo matatu-Kinondoni,Kigoma Mjini na Kahama- na kubakiza mawili ambayo ni Geita na Kigoma Kaskazini na kuahidi kuwa atatoa tamko rasmi la uamuzi wake Machi 28.

Zitto alisema akiwa na miaka 29 wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2005 alisema kuwa atakuwa mbunge wa kipindi kimoja, lakini watu hawakumuelewa na hata mwaka 2006 aliporudia kueleza hilo watu pia hawakumuelewa na mwaka 2007 aliposema kule Maswa kuwa hatogombea tena, hakueleweka. “Mwaka jana pia nilipoeleza kuwa sitogombea, watu hawakunielewa...

walipiga kelele niendelee, nikasema wengine mnawaita ving’ang’anizi na mnawapigia kelele watoke mie nawaomba nipishe hamtaki, lakini nilisahau ukiwa kiongozi maamuzi yako ni ya wananchi, nikaamua kuendelea kugombea,” alieleza.
Tags:

0 comments

Post a Comment