Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Katibu wa CCM achomwa kisu ofisini, afariki dunia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, Bahati Stepahano (49) amefariki dunia baada ya kuvamiwa ofisini kwake na kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alisema katibu huyo alivamiwa ofisini kwake katika Mtaa wa Nera jijini Mwanza na mtu ambaye hivi sasa anashikiliwa na polisi.

Kata ya Isamilo ni kata anayotoka Meya wa Jiji la Mwanza Leonard Bihondo. 

Ilielezwa kuwa mvamizi huyo, alifika katika ofisi za CCM akitaka kuonana na katibu huyo kwa madai ya kuwa na shida za kiofisi na baada ya kuruhusiwa kuonana naye alisikika wakibishana naye na baadaye alionekana akitoa kisu na kumchoma. Kamanda Sirro alisema tukio hilo, lilitokea saa 6:30 mchana.

  “Kwa mujibu wa mashuhuda baada ya kuona mabishano hayo waliamua kufuatilia na kumuona kijana huyo akitoa kisu na kumchoma katibu huyo, upande wa titi la kushoto na tumboni, baada ya kufanya hivyo inadaiwa alitoka mbio kutaka kutokomea, lakini wasamalia wema wakiwemo wafanyakazi wenzake na marehemu wamkimbiza na kumkamata akitaka kujitosa ziwani” alisema Kamanda Sirro.

Alisema polisi wameanza uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa za awali kwa watu walioshuhudia tukio hilo.

 Alisema kwa kuwa  wamemkamata  mtuhumiwa watatumia  mbinu za kijeshi na kikachero kutambua chanzo cha mauaji hayo.
Kufuaia kifo hicho, habari zimesikika kwamba mauaji hayo yanatokana na masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao kwa vile alikuwa haelewani na mwanasiasa mmoja ambaye mara kadhaa alikuwa akitaka katibu huyo ahamishwe katika kata yake kutokana na kutokubaliana na masuala yake ya kuhujumu wagombea wanaokuja kupingana naye.

  “Hii ni ishara kuwa siasa za sasa zimeanza kuchafuka, kwa vyoyote vile kifo hiki kinahusu masuala ya siasa, Mwanza tunaijua imekuwa na matukio ya mauaji hasa kwa watu wanapoguswa sana katika maslai yao . Siku chache kabla ya katibu huyo kuuawa kiongozi mwingine wa siasa katika kata hii amewahi kutishiwa kuuawa na kesi yake kumalizwa kinyemela na ofisa wa polisi,” alisema mmoja wa wanachama wa CCM.

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mwangi Kundya Rajabu amepokea kwa masikitiko kifo hicho na kusema kwa sasa chama kinasubili uchunguzi wa jeshi la polisi ili kubaini sababu za mauaji ya mtumishi wake.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akizungumza na gazeti hili, alisema  amestushwa na kwamba katibu alifarikia dunia wakati akipelekwa  Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Tags:

0 comments

Post a Comment