Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - CCJ yawasilisha maombi ya usajili kwa mbinde

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
CHAMA Cha Jamii (CCJ) jana kimewasilisha maombi ya usajili wa kudumu kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kwa mbinde baada ya ofisa masijala wa ofisi hiyo, Michael Paul awali kugoma kupokea maombi hayo.
Ofisa huyo aligoma kuzipokea fomu za chama hicho kwa maelezo kuwa mwanasheria wa msajili wa vyama vya siasa  na msajili mwenyewe hawakuwepo ofisini.

Kitendo hicho, kiliwafanya viongozi wa CCJ ambao ni  mwenyekiti Richard Kiyabo, Katibu Mkuu  Renatus Muabhi, Katibu Mwenezi Constantine Akitanda na Naibu Katibu Mkuu Ali Khatib Ali, kuzunguka ofisi moja hadi nyingine kutafuta msaada wa haraka.

Paul aliwaeleza viongozi hao, asingeweza kupokea maombi yao kwa kuwa hakukuwa na kiongozi yeyote anayestahili kupokea maombi hayo,  akiwemo Mwanasheria wa Msajili.

Kauli ya Paul ilipingwa vikali na viongozi wa chama hicho, wakiongozwa na Kiyabo ambaye alisema kazi iliyowapeleka hapo ni kukabidhi fumo za usajili wa chama hicho na kwamba wasingeweza kurudi na fomu hizo ambazo ni za wanachama wa mikoa 10 huku miwili ikiwa ni mikoa ya Kaskazini Pemba na Kusini Unguja.
 “Sisi kazi yetu iliyotuleta leo ni kuleta hizo fumo zenu, hatuwezi kurudi nazo ofisini kwa kuwa kazi  tuliyotakiwa  kufanya  tumeikamilisha, sisi hatumtaki msajili wala nani, sisi tunachotaka ni kuwakabidhi tu,” alisema Muabhi.
Baada ya kauli hiyo,  mchezo wa kuigiza ndipo ulipoanza baada ya viongozi hao wa CCJ  kulezwa na Paul kuwa hawezi kupokea maombi yao.

 “Mimi siwezi kupokea maombi yenu kwa sababu kwa mujibu wa taratibu, lazima mwanasheria wa msajili awepo pamoja na ofisa wa masijala,” alisema Paul aliyeonekana kuwa na hasira.
Baada ya majibizano ya dakika takribani 10, Paul alinyanyua simu ya mezani iliyokuwa mapokezi na kumpigia Mkuu wa Masijala,  Mwajuma Amiri ambaye alikuja na kuanza kuwasikiliza viongozi hao walioambatana na mlinzi wao.
Mwajuma baada ya kuwasikiliza viongozi hao, aliwataka walipie fomu hizo, Sh 50,000 kwenye ofisi inayohusika.

Walipofika kwenye ofisiya kulipia, mama mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliwaagiza  viongozi hao wakakabidhi fumo hizo kwa ofisa masijala, halafu  waende kulipia na kupewa stakabadhi yao.
Huku ikionekana kama ni mchezo wa kuigiza jinsi viongozi hao wa CCJ walivyokuwa wakihaha ofisi moja hadi nyingine hatimaye walitoa barua za mikoa kumi ambayo ni Arusha, Iringa, Mara,  Mwanza, Dodoma, Iringa, Pwani, Dar es Salaam, Kaskazini Pemba na Kusini Unguja na kumkabidhi  afisa masijala.

 “Katika mikoa hii tulitakiwa kuwa na wanachama 200, lakini kila mkoa tuna zaidi ya wanachama hao, kwa maana hiyo tumevuka malengo tuliyowekewa, hivi sasa tunachosubiri ni utaratibu wa ofisi ya msajili ambao ni kuhakiki kama kweli tuna wananchama wa idadi hiyo katika mikoa hii.

 “Ili kumpa kazi rahisi msajili wakati atakapokuwa akihakiki wanachama wetu tumeweka nyongeza ya wanachama 355, kutokana na hilo, hatutarajii kupata kikwazo kuhusu wanachama,” alisema.

Alisema msajili wa vyama huchaguliwa kwa busara na uadilifu, hivyo wanaamini kuwa kiongozi huyo ni mwadilifu na walimtaka atumie busara katika kushughulikia ujasili wa chama hicho ili kuwapa wananchi haki yao ya kikatiba.
Baada ya kupata usajili wa muda chama hicho,  kilipanda chati baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, Fred Mpendazoe kujiunga nacho
Tags:

0 comments

Post a Comment