IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MWANASIASA mkongwe nchini Edwin Mtei amemtabiria mabaya Rais Jakaya Kikwete kuwa atakabiliwa na upinzani mkali katika uchaguzi mkuu ujao tofauti na chama chake (CCM) kinavyodhani.
Mtei aliyasema hayo juzi mjini hapa katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili. Aliuponda mkakati wa CCM wa kukusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
"CCM itakabiliwa na upinzani mkali wakati wa uchaguzi mkuu tofauti na viongozi wake wanavyodhani. Hata Rais, Kikwete naye atakumbana na upinzani mkali tofauti na ushindi alioupta mwaka 2005," alisema Mtei.
Alisema matumaini ya CCM na Kikwete kuwa watapata ushindi kiurahisi ni ndoto, kwani wakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na wananchi kuchoshwa na utendaji wa mbovu chama hicho juu ya ahadi walizotoa mwaka 2005 ambazo hazijatekelezwa.
Kuhusu hatua ya CCM kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, Mtei ambaye pia ni muasisi wa Chadema huo alisema wameiga kutoka Chadema, kwa sababu sera za CCM haziwezi kuvutia wananchi.
Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu alisema mkakati huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete, hauwezi kuwavutia wala kuwashawishi wananchi kuichangia CCM na kuwa haina jipya.
"Nawaonea huruma CCM, kwani hawana jipya, hawawezi kubuni kitu kipya cha kwao. Sisi tulianza kuchangia fedha kwa njia ya uwazi na wao wamefuata nyayo; kwa kweli CCM hawana jipya,"alisema Mtei
Alidai ya kuwa sera za CCM haziwezi kuwashawishi wananchi kukichangia chama hicho na kuwa serikali CCM inayojipambanua kupiga vita rushwa imeshindwa kudhibiti mafisadi wanaotajwa ndani ya chama hicho.
"Sera za CCM kamwe haziwezi kuwavutia wananchi hadi wakichangie chama hicho, serikali inadai inapiga vita ufisadi, wakati serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwadhibiti mafisadi na wahujumu uchumi walio ndani ya chama chao,"alisiitiza Mtei.
Akizungumzia fedha za Mfuko wa Kichocheo cha Maendeleo ya Jimbo(CDCF) zinazotarajiwa kugawanywa mwishoni mwa mwezi huu, Mtei alisema fedha hizo zitaangukia kwenye matumzi ya siasa badala ya mandeleo ya majimbo kama ilivyokusudiwa.
"Huwezi kutoa pesa kipindi hiki, hizi ndizo siasa za nchi hii. Hizi pesa za mfuko wa kichocheo cha maendeleo ya jimbo ni za siasa si za maendeleo, kwani hazina jipya,"alisema Mtei bila kufafanua.
Katika hatua nyingine Mtei pia aliishambulia CCM akidai ya kuwa imeshindwa kujali maslahi ya wananchi na kuangalia maslahi ya watu wachache ambapo alisema kuwa umasikini wa Watanzania umesababishwa na chama hicho.
You Are Here: Home - - Mtei amtabiria mabaya Kikwete, CCM
0 comments