Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wabunge wa CCM kumuunga Slaa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter WABUNGE wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walikutana juzi jioni kukubaliana kuunga mkono mapendekezo ya Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa aliyowasilisha kwenye kamati ya uongozi ya bunge kutaka bunge lipitie upya sheria ya gharama za uchaguzi na kuifanyia marekebisho kabla ya kuanza kutumika.

Vile vile, walikumbushwa mikakati mbalimbali ikiwemo wa kulinda kura zao wakati wa uchaguzi kwa kuweka mawakala waaminifu ili zisipotee kwa wapinzani.

Habari za ndani ya kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM, ambacho huongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama mwenyekiti, kilianza saa 11:50 jioni muda mfupi baada ya kumalizika kwa bunge na kumalizika saa 2:00 usiku.

Mbali na kuzungumzia mkakati huo wa kulinda kura zao pia ulielezwa na kufafanuliwa mapendekezo ambayo Dk Slaa amewasilisha na kuelezwa kuwa wanapaswa kukubaliana nayo kwa vile hayana athari katika chama chao.

"Tulipitia mkakati wa chama wa mbinu za kulinda kura katika uchaguzi mkuu ujao ili zisipotee kwa wapinzani," alieleza alieleza mmoja wa wabunge wa CCM.

Kuhusu mapendekezo ya Dk Slaa chanzo hicho kilibainisha, “Kwa kifupi tumejadili mapendekezo yote yatakayoletwa na Dk. Slaa na kukubaliana nayo. Tumekutana kuangalia iwapo yanatuathiri… ndiyo hivyo tumekubaliana nayo na sheria hiyo itajadiliwa upya bungeni."


Hata hivyo, Spika wa Bunge Samuel Sitta aliliambia Mwananchi Jumapili wiki hii kuwa, " Tumeona katika sheria hii mambo mengi yako kinadharia, kwa mfano; sheria inasema kuwe na wajumbe wa kampeni wasiozidi 20 kwa mbunge na 10 kwa diwani na wagombea hao wawe wameidhinishwa na DAS au WEO."



"Hili ni jambo jema, lakini tafsiri yake ni kwamba serikali sasa itakuwa na ruhusa ya kukubali au kukataa nani aingie kwenye kampeni hizo na nani asiingie; na kama hiyo ndiyo tafsiri, kimsingi inaleta shida." 

Spika Sitta alifafanua kuwa katika bunge hili, wabunge watazitazama tena kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo na kuzifanyia marekebisho. 

Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa amewasilisha mapendekezo hayo kutokana na kile alichodai kuwa Rais Kikwete amedanganywa na kusaini sheria hiyo kimakosa.


Alisema aliamua kuliwasilisha suala hilo kwanza kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ili kama angepuuzwa, alifikishe suala hilo bungeni mwenyewe kwa namna anayoona inafaa. 

"Mapambano ndio yameanza; mimi ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge na leo (jana) tulikuwa na kikao, nimehoji suala hilo kabla sijalifikisha bungeni kwa namna ambayo nitaona inafaa," alisema Dk Slaa.



"Bado nasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu amedanganya kwa kusema vifungu hivyo viko sahihi kwa kuwa Ofisi ya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera na Uratibu wa Bunge-, Phillip) Marmo ndio iliyovifanyia marekebisho. Ofisi ya Marmo haina mamlaka ya kubadili vifungu vya sheria iliyopitishwa na Bunge. 

Alisisitiza kuwa kilichojadiliwa bungeni ni vikundi vya sanaa na Bunge liliagiza viingizwe vifungu vya ufafanuzi na sio mabadiliko ya vifungu.
Tags:

0 comments

Post a Comment