Waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameshutumu azimio ambalo limepitishwa na bunge la Marekani linalodai majeshi yake yalitekeleza mauaji ya halaiki ya waarmenia wakati wa vita vya dunia vya kwanza.
Erdogan amesema nchi yake inashutumiwa kwa uhalifu ambao haikutekeleza.
Ameongezea kuwa hatua hiyo ya Marekani itadhuru uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Tayari Uturuki imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Marekani.
Mwandishi wa BBC anasema swala hili ni nyeti sana nchini Uturuki ambayo ni mshirika wa karibu wa Marekani na mwanachama mwenza katika muungano wa mataifa ya NATO
0 comments