ZIARA za kikazi zilizofanywa kwenye mikoa mbalimbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, zimekichefua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma kwa shughuli za Chama Cha Mapinduzi (CCM).Pamoja na hayo, CHADEMA kimelaani na kumtaka Pinda kuwajibika kutokana na kukiuka Katiba, sheria na misingi ya utawala bora wenye demokrasia ya vyama vingi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Vijana CHADEMA na kusainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo, vipengele vya Katiba vilivyovunjwa na Waziri Mkuu ni Ibara ya 13 kifungu cha (4) kinachopiga marufuku ubaguzi.
“Kifungu hicho kinasema ‘Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.
“…Kifungu kingine ni kile cha tano kinachofafanua kuwa, ubaguzi ni pamoja na ubaguzi wa kisiasa. Kadhalika CHADEMA inamkumbusha Waziri Mkuu Pinda kwamba Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 inataja misingi ya maadili ya kufuatwa pamoja na mambo mengine kifungu cha sita kipengele (i) kinakataza mali za serikali kutumiwa kwa lengo na manufaa binafsi ya kiongozi husika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Tumbo, akiwa Dodoma Pinda aliwataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kujua salamu za CCM, kitendo chake cha kuchangia sh milioni tano kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Manispaa ya Moshi kwa ajili ya kambi za vijana.
Alisema akiwa kwenye ziara ya kiserikali Waziri Mkuu alitoa maneno ya kuwataka wananchi wa Igunga mkoani Tabora kumchagua tena Mbunge wao Rostam Aziz, kwa kuacha kusikiliza maneno yanayosemwa bungeni.
Kwa kauli hizo, Tumbo ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuzifafanua ama kuzikanusha kauli hizo ili kuondoa dhana ya ubaguzi kwa vyama vingine vya siasa na kuwaomba radhi Watanzania kwa sababu ametumia muda wa kazi za kiserikali kutekeleza majukumu yake ya kichama.

0 comments