Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Ndege ATC yaanguka Mwanza

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Habari toka mwanza zinasema ndege aina ya boeing 737 ya atcl iliyokuwa ikitokea dar asubuhi hii imepata ajali ndogo wakati ikitua katika uwanja wa mwanza ikiwa na abiria kama 40 hivi.

Hakuna aliyepata madhara na abiria wote na wafanyakazi wako salama, ndege hiyo yenye namba ya mruko tc 100 ilipata dhahama hiyo wakati ilipotua kwenye bwawa kubwa la maji lililotuama kwenye njia ya kutulia (runnaway) uwanjani hapo kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

Inasemekana maji yaliingia kwenye injini moja na ambayo ikazimika na kuifanya ndege iache njia na kwenda pembeni kiasi cha mita 300 hivi.
Tags:

0 comments

Post a Comment