Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Daktari mbakaji apewa UCHUNGAJI!

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Dk. Paul ambaye yupo nje kwa dhamana katika kesi yake inayoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar, alitunukiwa cheti hicho juzi, Februari 27, 2010 katika Kanisa la The Pool of Siloam Church, lililopo Mbezi Makonde, jijini.




Baba wa Kiroho wa kanisa hilo, Mchungaji Eliah Mnuo ndiye aliyemkabidhi cheti cha utumishi wa Mungu Dk. Paul, hivyo kumpa baraka zote za kuwaongoza kondoo wa bwana.

Mchungaji Dk. Paul, alikabidhiwa cheti chake majira ya saa 10 alasiri ambapo kabla na baada yake, walitunukiwa vyeti wachungaji wengine waliohitimu masomo katika kanisa hilo.

Kiongozi wa kanisa hilo, Mtume Zebedayo N. Eliya alipoulizwa, alikiri kufahamu kwamba Dk. Paul ni mfanyakazi wa Hospitali ya Marie Stopes lakini akadai kuwa alikuwa hajui kama ana kashfa ya kumbaka mgonjwa.

Hata hivyo daktari huyo amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi pamoja na mwenendo wa kesi mahakamani.

Alipohojiwa mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho, Mchungaji Dk Paul na kuuulizwa kisa cha kukubali kutunukiwa cheti cha uchungaji wakati ana tuhuma nzito mahakamani alisema haangalii sifa za duniani, “ninachofanya mimi ni kumtumikia Mungu, siangalii sifa za duniani,” alisema
Tags:

1 comments

  1. Anonymous says:

    Huo ni uzushi..acha kuchafua kanisa!
    tafuteni habari za maana zenye ushuhuda..

Post a Comment