IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MGOGORO wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Tanga umeingia katika hatua nyingine baada ya viongozi wa ngazi ya walei kumkabidhi barua Askofu wake Dk Phillip Baji kumtaka ajiuzulu ndani ya siku tano kuanzia jana.
Walei hao, kutoka makanisa au dinari tisa kati ya 14 ya Dayosisi hiyo, mkoani Tanga, walimkabidhi barua Askofu Baji, jana saa 6:10 mchana baada ya kuandamana hadi makao makuu ya kanisa hilo mjini Korogwe.
Wakiwa na jazba, walei hao walipofika makao makuu ya kanisa hilo,
yaliyopo Old Korogwe mjini hapa, waliomba kukutana na Askofu Baji ili wamkabidhi barua huku wakisisitiza kuwa hawahitaji kuwa na mazungumzo naye.
Madai yaliyotolewa katika barua hiyo ya kumtaka Dk Baji ajiuzulu, yalikuwa saba likiwemo la ubadhilifu wa fedha za kanisa hilo.
Akisoma tuhuma za Askofu Baji, Katibu wa timu iliyoteuliwa na jumuiya ya dinari tisa, Augustino Sekiola alisema tuhuma ya kwanza ni kusababisha dayosisi yao kuingia katika madeni makubwa yasiyolipika.
Tuhuma namba mbili kwa mujibu wa barua iliyosomwa na Katibu huyo ni Askofu Baji kujihusisha na ubadhilifu wa kutumia fedha za michango mbalimbali ya kanisa hilo, tatu kuisababishia dayosisi kuwa maskini na nne anatuhumiwa kutafuna fedha za wahisani mbalimbali hadi kufikia hatua ya kusitisha ufadhili katika kanisa hilo.
Sekiola alisema tuhuma ya tano ni baadhi ya wakristo wamelihama
kanisa la Anglikana na kuingia katika madhehebu mengine na makasisi kuhamia dayoisisi nyingine, sita anatuhumiwa kuiongoza
dayoisisi hiyo kibabe na kidikteta kuanzia alipoingia
madarakani miaka tisa iliyopita hadi sasa.
“Wakristo katika dayosisi kutokuwa na imani na wewe kiroho kunatokana na tabia yako mbaya, rejea kashfa ya ufuska iliyokukumba mwaka 2004 na mambo mengine,†alisema Sekiola.
Akizungumza baada ya kupokea waraka huo, Askofu Baji
alisema ana haki ya kusema, lakini hawezi kuwajibu walei hao kwa kuwa masuala kama hayo, kikatiba yanapaswa kuzungumzwa katika kikao cha halmashauri kuu ya kudumu.
“Sitaki tukio lolote liendelee katika eneo hili huku waandishi wa habari wakishuhudia kinachoendelea samahani sana,â€alisema Askofu Baji na kusababisha waandishi wa habari waliokusanyika ndani ya kanisa Makao makuu ya Dayosisi hiyo, kutoka nje.
Baadhi ya waandishi wa habari walibaki ndani ya kanisa hilo,
bila kutambulika na Askofu Baji alisema ikibainika
hana kosa hatakuwa tayari kuendelea na wadhifa huo.
“Barua hii kabla ya kuletwa hapa imeshasambazwa kwa njia mitandao ya Internet duniani nzima, lakini kati yenu hakuna anayeweza kuthibitisha tuhuma hizi, alisema Dk Baji
You Are Here: Home - - Anglikana Tanga yawaka moto. Waumini wamtaka askofu ajiuzuru ndani ya siku tano
0 comments