Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - CCJ wamvaa John Tendwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter



Askari wa usalama barabara Manispaa ya Morogoro aliyetambuliwa kwa jina moja la Mandela akisimamisha magari ili wananchi wavuke katika tuta lililopo barabara ya Lumumba stendi ya daladala yaendayo nje ya mji huo. Picha na Juma Mtanda




WAHOJI ALIKUWA WAPI KUWAZUIA KAMA WALIKUWEPO MIAKA MIWILI NYUMA

Ramadhan Semtawa

BAADA ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutangaza kuanza uchunguzi wa kuona kama Chama Cha Jamii (CCJ) kilifanya siasa miaka miwili kabla ya usajili; viongozi wa chama hicho wamejibu mapigo kwa kuhoji kwamba; ofisi ya msajili na vyombo vya usalama vilikuwa wapi, hadi chenyewe kifanye siasa kinyume cha sheria.

Mapigo hayo ya CCJ yanatokana na kauli ya msajili huyo aliyoitoa juzi kabla ya kuwakabidhi cheti cha usaji wa muda kwamba; ofisi yake imepata taarifa kuwa CCJ ilianza kufanya shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita na kusisitiza kuwa ikithibitika atakifutilia mbali.

Kauli hiyo ya kitisho inayoiweka CCJ njia panda, jana ilijibiwa vikali na Katibu Mkuu wake, Renatus Muabhi aliyehoji kwamba, kama ofisi hiyo ya msajili iko makini ilikuwa wapi kuigilia kati wakati huo kama kweli chama hicho kilianza kufanya shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita?

Muabhi licha ya kumshangaa Tendwa, alisema kama ikithibitika ni kweli basi msajili huyo na wasaidizi wake na hata baadhi ya vyombo vya usalama vitapaswa kuwajibika.

Juzi Msajili akizungumza na kituo cha ITV alirusha kombora kwa CCJ siku moja kabla ya kukipatia usajili na kuweka bayana kwamba, ofisi yake imepata taarifa hizo za chama kujipanga kisiasa kabla ya usajili na kuonya atakifuta.

Akijibu kombora Muabhi alisema: "Msajili na vyombo vya usalama vilikuwa wapi? Mbona msajili alijua taarifa zetu kabla ya kupeleka taarifa za maombi ya usajili ofisini kwake?" alihoji Muabhi na kuongeza:

"Hiyo siasa tulikuwa tukiifanya katika nchi gani, hivi kweli Tanzania hii unaweza kufanya siasa kwa miaka miwili kinyume cha sheria bila kujulikana?"

Kwa msisitizo, Muabhi alisema mpango huo ni njama za kukihujumu na propaganda chafu zisizokuwa na mantiki dhidi ya CCJ baada ya kuona mwelekeo wake kisiasa unaelekea kuungwa mkono na Watanzania wengi.

Muabhi alisema chama hicho lazima kitakutana na mawimbi mazito sawa na ya bahari, lakini hakitarudi nyuma, kitajiimarisha na kushikamana na Watanzania wazalendo.

Alisema tayari kimepanga vema ratiba yake ya kusaka idadi ya wanachama 2,000 nchini kote ambayo inaonyesha itakuwa katika mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Pemba, Mara, Mbeya, Shinyanga na Iringa.

Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba, kadi zao kwa wanachama zitauzwa kwa bei ya chini ambayo haitazidi Sh 400 na baadhi wasiojiweza watapatiwa bure baada ya utaratibu kukamilika.

CCJ ujio wake unaangaliwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa kama tishio kwa CCM na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais hapo Oktoba.

Tayari Spika wa Bunge Samuel Sitta, aliwahi kusema kwamba, haoni tatizo la kusajiliwa CCJ huku pia akisema hawezi kuzuia watu kumuhusisha na chama hicho kama mgombea hapo Oktoba.

CCJ imekuwa ikitikisa nchi tangu taarifa zake kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, kwani kuna majina makubwa yanatajwa kuwemo akiwemo Spika Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, John Malecela, lakini wote wamekanusha.

Hata hivyo, mwasisi wa CCM Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema bila CCM madhubuti nchi itayumba na kwamba, upinzani wa kweli utatoka ndani ya chama hichi, onyo ambalo wadadisi wa mambo ya siasa wanaona kuwa linakaribia.
Tags:

0 comments

Post a Comment