Maelfu ya raia wa Eritrea wameandamana katika maandamano yaliyoratibiwa kwenye nchi za Australia, Switzerland na Marekani wakipinga vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Raia wa Eritrea wanaoishi Uigereza wameimbia BBC kuwa vikwazo hivyo sio vya haki na ni matusi kwa taifa lao.
Inaarifiwa maandamano hayo yamechochewa na serikali ya Eritrea na huenda baadhi ya mawaziri wamesafiri hadi Ulaya kuratibu maandamano hayo.
Vikwazo hivyo viliwekea Eritrea na Umoja wa Mataifa baada ya taifa hilo kulaumiwa linawadhamini wanamgambo nchini Somalia wanaopigana na serikali ya mpito ya nchi hiyo.
Baadhi ya vikwazo hivyo ni kuzuia taifa lolote mwanachama wa Umoja wa Mataifa kuiuzia Eritrea silaha, vikwazo vya kusafiri na kuzuiwa kwa fedha zilizowekwa ng'ambo na viongozi wa serikali hiyo.
0 comments