Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mawaziri wa JK kuburuzwa kortini. ni Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MWENYEKITI wa chama kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anaandaa utaratibu wa kuwafungulia mashtaka Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo kwa kuidharau Katiba.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila alisema kitendo cha viongozi hao wawili kwa nyakati tofauti kueleza kuwa suala la mgombea binafsi haliwezekani na linahitaji lipelekwe kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni ni kuvunja Katiba.
“Utaratibu wa kuwasimamisha kizimbani Marmo na Membe kwa kuvunja Katiba na sheria kwa kuthubutu kuifanyia jeuri na dharau mahakama ya nchi uko palepale,” Mtikila alisema.
Mwenyekiti huyo wa DP alisema kwa sasa wanasheria wake wanashughulikia kesi nyingine zipatazo tisa za Kikatiba lakini suala hilo litashughulikiwa hadi haki hiyo kwa Watanzania ipatikane.
Alisema hoja ambazo zimekwishatolewa na mawaziri hao pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu, ni porojo na haziwezi kuathiri utendaji wa mahakama.
Aliukosoa utetezi wa Waziri Marmo kwamba muda hautoshi kwa kuandaa mazingira ya mgombea binafsi kwa vile suala hilo linahitaji umma kushirikishwa na kusema hiyo ni haki ya Kikatiba, haihitaji umma kuulizwa iwapo wanaitaka.
Mtikila alisema amri ya mahakama kuruhusu mgombea binafsi ilitolewa Mei 5, 2006 na kuwatuhumu watendaji wa serikali akiwemo mwanasheria mkuu kufanya njama za kutotekeleza amri hiyo kwa miaka minne sasa.
“Pili, hakuna mabadiliko kufanywa katika Katiba wala mahakama haiamuru hivyo kwa sababu Katiba ndiyo inayotoa haki hii kwa kila raia hasa Ibara ya 21 (2)...mahakama tu ndiyo inayotoa haki nchini ya kutafsiri sheria pamoja na Katiba ...siyo Marmo, Membe wala Rais Jakaya Kikwete,” alisema.
Akinukuu maneno ya Waziri Membe aliyoyatoa kwa mabalozi baada ya kukutana nao katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mchungaji Mtilila alisema hatua ya kuwataka mabalozi wavute subira juu ya suala la mgombea binafsi ni kuliuza taifa.
Katika hilo, mwanasiasa huyo anayeongoza kwa kufungua kesi nyingi dhidi ya serikali, alisema waziri huyo ameuza uhuru wa taifa kwa kitendo chake cha kuwanyima Watanzania haki yao huku akijadiliana na wanadiplomasia hao.
“Membe amethibitisha tabia inayowachukiza wananchi kwamba wanaotawala nchi yetu hawana ridhaa ya wenye nchi, bali wanajisalimisha kwa mataifa makubwa,” alisema.
Alisisitiza kwamba suala la kugombea uongozi ndani ya nchi ni nyeti na ni la utaifa ambalo kulitafutia uhalali kwa mataifa mengine ni kuuza uhuru wa nchi, kosa alilolifananisha sawa na uhaini.
Aliushutumu uongozi wa Rais Kikwete kwa kutaka kuhujumu haki hiyo na kutabiri kutokea machafuko yatakayoifanya Tanzania kutengwa na jumuiya za kimataifa.
Alisema mbinu ya kuzima suala la mgombea binafsi inayofanywa na watendaji wa Rais Kikwete inatokana na hofu ya kumpata mgombea atakayechuana naye katika kinyang’anyiro cha urais Oktoba.
“Rais Kikwete hata akifaulu kuzima ushindani ndani ya chama chake, ataibuka mgombea binafsi na wanachama wote watamfuata na kuiacha CCM inamfia mikononi,” alisema.
Aliongeza kwamba baada ya usajili wa Chama cha Jamii (CCJ), hatma ya CCM ilianza kuwa mashakani kutokana na ukweli kwamba ilianza kutikisika.
Tags:

0 comments

Post a Comment