Serikali ya kijeshi iliyofanya mapinduzi nchini Niger wiki jana, imemtangaza waziri mkuu mpya Mahamadou Dandah ambaye ni raia.
Dandah alikuwa waziri wa habari katika utawala wa mwaka 1999 ulionyakuwa mamlaka kwa mapinduzi. Atahudumu hadi wakati ambapo uchaguzi ambao umeahidiwa na serikali hiyo ya kijeshi utafanyika.
Aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mamadou Tandja, alichaguliwa kuiongoza Niger katika uchaguzi wa kidemokrasia lakini alikataa kuondoka muhula wake ulipokwisha mwezi Desemba mwaka jana, hali iliyosababisha utawala wake kupinduliwa.
Kwa hivi sasa Tandja na waliokuwa mawaziri wake wanazuiliwa na jeshi na inaarifiwa kuwa wako katika hali nzuri. Shirika la msalaba mwekundu limeiambia BBC kwamba limeridhishwa na jinsi viongozi wa kijeshi wanavyomlinda rais huyo wa zamani na mawaziri wake.
0 comments