Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown anatarajiwa kuomba msamaha rasmi kwa namna Uingereza ilivyowarejesha watoto zaidi ya laki moja katika makoloni yake ya zamani.
Hatua hiyo ya Uingereza ilichukuliwa chini ya mpango wenye utata wa kuwarejesha makwao wahamiaji miaka arobaini iliyopita.
Watoto wengi walichukuliwa kutoka familia zao kwa nguvu na kupelekwa Australia, Canada na nchi nyingine za Jumuiya ya madola.
Inasemekana badala ya watoto hao kupata maisha bora, waliteswa kwenye makao ya kuwatunza na walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwenye mashamba.
Waathiriwa sitini wamerejea London kushuhudia Waziri Mkuu Brown akiomba msamaha huo.
Mwezi Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu wa Australia, Kevin Rudd, pia aliomba msamaha kwa waathiriwa hao waliojulikana kama raia wa Australia waliosahaulika.
0 comments