Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Sheria kuhusu Rais yabadilishwa Nigeria

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Idadi kubwa zaidi ya wabunge katika bunge la senate, wamepiga kura kumpa Rais muda wa wiki mbili, kutangaza ikiwa hawezi kutekeleza majukumu yake.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo, Rais atahitaji kuliandikia bunge barua rasmi kwa muda huo iwapo atachukua likizo ya zaidi ya wiki mbili au atakuwa na matatizo ya afya.
Baada ya kupokea barua hiyo bunge litapiga kura kumruhusu makamu wa Rais kuwa kaimu kwa muda ambao Rais hatakuwapo.
Hakuna shaka kuwa hatua hiyo inafuatia msukosuko wa kisiasa ambao ulitokea wakati ambapo Rais Umaru Yar'Adua aliondoka kwenda kwa matibabu nchini Saudi Arabia.
Makamu wa rais Goodluck Jonathan alipewa mamlaka ya kuwa kaimu wa rais, hatua iliyopingwa na baadhi ya wanasheria na wanasiasa kwa sababu haikuruhusiwa kikatiba.
Baadhi ya wanaomuunga mkono Rais Yar'Adua, wanasema makamu wa Rais hawezi kuendelea kuwa kaimu, kwani Rais mwenyewe amerejea nyumbani. Lakini ikulu ya Rais imetoa taarifa kuwa bwana Jonathan anaweza kuendelea kushikilia wadhifa huo.
Baadhi ya wabunge na wanaharakati wengine wanamtaka Rais huyo ajiuzulu mara moja kwani wanasema,hana tena uwezo wa kuongoza nchi.
Tags:

0 comments

Post a Comment