Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Walemavu Wachapana mbele ya Waziri mkuu Mizengo Pinda

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Walemavu wazichapa mbele ya Pinda

KUNDI la watu waliochanganyika na wenye ulemavu jana lilifanya vurugu kwa kufanya uharibifu wa mali mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakigombea vinywaji na baadaye kudai posho kwa nguvu kwenye hafla ya chakula cha mchana...


Hafla hiyo fupi iliandaliwa na mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, ambaye ana kawaida ya kuandaa chakula cha mchana kila mwaka kwa ajili ya watu wenye ulemavu, lakini safari hii hisani yake haikumalizika kwa amani.

Vurugu ziliibuka muda mfupi baada ya Waziri Pinda kuanza kutoka ukumbini baada ya kushiriki chakula na watu wenye ulemavu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Chupa za vinywaji na meza zilizowekewa vyakula na vinywaji zilivunjwa, watu walisukumana na kupigana wakati vurugu kubwa zilipotokea kwenye maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya kutoa huduma ya vinywaji.

Mwananchi lilishuhudia baadhi ya watu wakiwa wamekandamizwa chini huku wakipatiwa kipigo kutoka kwa wenzao waliokuwa wakiwasukuma ili watoke eneo la vinywaji, wakionekana hawaamini kuwa kulikuwa na vinywaji vya kutosha.

Hali hiyo iliwalazimisha wafanyakazi wa IPP ambao jana ndio walikuwa wahudumu kwenye hafla hiyo kukimbia na kuacha kila kitu kutokana na kuzidiwa nguvu na kundi hilo la watu.

Baadhi ya wafanyakazi wa IPP waliiambia Mwananchi kuwa wanashangazwa na vurugu hizo kwa sababu vinywaji vilikuwepo vya kutosha kwa ajili ya watu hao, lakini wakaongeza kuwa watu ambao hawakukusudiwa kwa hafla hiyo, ndio waliovamia na kufanya vurugu hizo kwa kuwa hali kama hiyo haijawahi kutokea katika miaka yote ambayo Mengi huandaa chakula cha mchana.
Tags:

0 comments

Post a Comment