Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wabunge waukataa muswada

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter WABUNGE leo wameukataa muswada wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wa mwaka 2009.

Hoja za wabunge zimemlazimisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba aurudishe muswada huo katika Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili ukarekebishwe.

Naibu Spika wa Bunge, Anna Makinda, amelazimika kutumia madaraka yake kukatisha mjadala kuhusu muswada huo kwa kutompa Kiongozi wa Shughuli za Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, fursa ya kuchangia.

Hali hiyo haikutarajiwa, Makinda amewaeleza wabunge kuwa anaendesha Bunge anavyoona yeye.

Mohamed amewaeleza waandishi wa habari kuwa, kwa madaraka aliyonayo bungeni, Makinda anamdhalilisha kwa kuwa si mara ya kwanza kumzuia asichangie.

Waziri Simba ametumia Kanuni ya 87 ya Bunge kifungu kidogo cha kwanza kuliomba Bunge auondoe muswadsa aliouwasilisha ili aurudishe kwenye kamati.

Makinda aliwahoji wabunge kama wanakubali wakasema ndiyo, na amewataka wahusika wote washiriki kuuboresha muswada huo na utakapokuwa tayari apewe taarifa.
Tags:

0 comments

Post a Comment