Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kampuni za simu, wateja kubanwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta wa mwaka 2009.

Rais akisaini muswada huo kampuni za simu zitatakiwa kujisajili katika Soko la Hisa ili kuweka wazi mapato yao na kuwawezesha watanzania kununua hisa.

Wakati wakiujadili muswada huo , wabunge walidai kuwa kampuni za simu zimekuwa zikifanya udanganyifu na kuwanyonya watanzania kwa kupitia huduma za ofa.

Wabunge hao wamedai kuwa, kupitia ofa hizo kampuni hizo pia zimekuwa zikiinyima Serikali mapato yake halisi.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla, amesema wakati akiwasilisha muswada huo kuwa, lengo la muswada huo ni kutunga sheria itakayoshughulikia na kusimamia mawasiliano ya elektroniki na posta na kuwawezesha wadau kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo kwa mtindo wa ushindani.

Waziri Msolla amesema, maudhui ya muswada huo ni kuboresha matumizi ya simu za mkononi, kuweka udhibiti wa wizi wa simu za mkononi, kuruhusu matumizi ya digitali, kumuwezesha kila mtumiaji kupata anuani na kusajiliwa ili kuzuia wizi wa simu, na kwamba, awali hakukuwa na sheria kama hiyo.

Amesema, muswada huo una vipengele vingi vinavyozidhibiti kampuni za simu kikiwemo kinachozitaka zijisajili katika soko la hisa baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu ili kuiwezesha Serikali kupata mapato halali na kuwawezesha watanzania kununua hisa katika kampuni hizo.

Amesema, muswada huo umeipa Mamlaka ya Mawasiliamo Tanzania (TCRA), uhuru wa kudhibiti masafa ya redio zote nchini ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuyafuta iwapo sheria hiyo itakiukwa, na usajili wa simu kadi.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, mtu akitumia simu kadi isiyosajiliwa atatozwa faini ya shilingi milioni moja na kuweka kanuni zitakazoainisha aina ya huduma za posta kwa lengo la kuboresha huduma hiyo na kuiweka karibu na wananchi.
Tags:

0 comments

Post a Comment