Habari kutoka Bukoba zinasema wananchi wa eneo hilo wamelazimika kukimbia makazi yao na kwenda kujificha vichakani kwa zaidi ya mwezi mmoja wakihofia kupata kichapo polisi na mgambo wanaodaiwa kumlinda mkoloni huyo.
Wananchi wengi wanadai wameshindwa kujishughulisha na kazi za kilimo kutokana na vitisho, vipigo na kuwekwa rumande, huku wakibambikizwa kesi mara wanapokutwa katika eneo hilo ambalo Maintland amelifanya kama nchi yake ndani ya Bongo.
Kwa upande wake Maintland, alisema katika eneo hilo hakuna raia wa Tanzania anayeishi kwani wote waliopo ni wakimbizi kutoka nchini Burundi.
Alidai watu hao wanatumwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Willson Masilingi kuendelea kuishi katika ardhi yake ili aendelee kupata wapiga kura wengi kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.


0 comments