Msemaji wa serikali ametangaza kuwa, Ali Hassan al-Majid, aliyekuwa afisa wa Iraq ajulikanaye kama Chemical Ali amenyongwa.
Majid, aliyekuwa mtekelezaji wa sheria katika uongozi wa Saddam Hussein na pia ndugu yake, awali alihukumiwa kifo mara nne kwa mfululizo wa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Mwezi Januari, alihukumiwa kifo kwa kutoa amri ya kuua kwa kutumia gesi katika mji wa Kikurdi uitwao Halabja mwaka 1988.
Inaaminiwa takriban watu 5,000 waliuawa katika shambulio hilo.
0 comments