IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Pamoja na kwamba viongozi wengi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameeleza kutokuwa na wasiwasi wa kumeguka kwake, ni dhahiri kuwa homa ya kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) imezidi kupanda huku vyombo vya usalama vikihaha kutaka kujua vigogo walioko nyuma ya chama hicho.
Chama hicho kuliwasilisha barua ya kuomba usajili wa muda katika Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa tangu, Januari 19 mwaka huu kimekuwa gumzo, na tayari harakati za wazi na za siri za kukitaka makali zimeanza.
Mojawapo ya mikakati hiyo ni kuwatumia mashushushu kuwachunguza waanzilishi wake wa wazi na wengine wanaodaiwa kuwa nyuma ya pazia.
Habari zilizotufikia kutoka chano kimoja cha habari cha kuaminika,zimesema mashushushu kutoka vyombo mbalimbali vya serikali ya CCM, wanahaha kupata majina ya wale wanaotajwa ‘vigogo wa CCM’ walioko nyuma ya chama hicho.
Baadhi ya maeneo ambao wanausalama hao wametega masikio yao ni pamoja na kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wabunge, ambako inasemekana waanzilishi wengi wa CCJ wapo.
Waandishi wawili wa habari wamethibitisha ama kupigiwa simu au kuulizwa ana kwa ana na watu wanaojitambulisha kwa aina tofauti, wakitaka kujua majina ya wahusika wa chama hicho kipya.
“Kuna mtu mmoja wa usalama namfahamu, kanipigia simu kuuliza kama nawafahamu watu walioanzisha CCJ, alisema mwandishi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kinachowachanganya wakubwa wa CCM ni jinsi chama hicho kilichosajiliwa na watu wasiokuwa na majina kilivyoweza kufahamika haraka hata kabla ya kupata cheti cha usajili wa muda, na jinsi kilivyoweza kuvivutia vyote vya habari, tofauti na ilivyo kwa vyama vingine.
Ingawa Msajili wa vyama vya siasa, Bw. John Tendwa ameshasema kuwa vipo vyama vingi zinavyoomba usajili, kinachowashangaza wachunguzi wa mambo ya kisiasa, ni kwa jinsi gani CCJ inavyouliziwa kila mara na kuhusishwa na kongamano la kupambana na ufisadi linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Februari 13, mwaka huu.
Mbali na waandishi wa habari,mmoja wa wabunge amelithibitishia Majira kwa amehojiwa na watu aliowaita wa usalama, wakitaka kujua kama wanawafahamu wahuska walio nyuma ya CCJ na wakati huo bado ni wanachama wa CCM.
Akizungumza na chanzo hicho cha habari mbunge huyu ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema ameulizwa maswali mengi na mitego, iwapo naye ni mmoja wa waanzilishi wa chama hicho.
Alisema watu hao ambao hujitambulisha kama ni waandishi wa habari wamekuwa wakimpigia simu kwa nyakati tofauti na kumuuliza kuhusu chama hicho, lakini anapowaomba kukutana ana kwa ana nao ili awezea kutoa msimamo wake hukwepa kufanya hivyo.
Hata hivyo, mbunge huyo alisema kinachofanyika sasa ni kutimia kwa utabiri wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere alioutoa kuwa ‘upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM’ na sasa umefika wakati wake.
Alisema kuwa mambo yote yanayotokea ndani ya CCM yanatokana na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa CCM kushindwa kuchukuwa maamuzi magumu ndani serikali na katika chama.
Alisema idadi kubwa ya wabunge na wananchi wengi wamechoshwa na kuendeshwa na watu aliowaita wenye fedha wanaojali maslahi yao bila kungalia maslahi ya taifa kwanza.
You Are Here: Home - - Mashushushu wahaha kuwajua wamiliki CCJ!
0 comments