Chama tawala cha Mapinduzi, Visiwani Zanzibar, katika mkutano wao wa mwishoni mwa wiki yaonesha kimekubaliana na hoja itakayowasilishwa na mkuu wa upinzani wa chama cha CUF katika Baraza la wawakilishi visiwani humo ambayo huenda ikapelekea siku za mbele kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa katika visiwa hivyo. Hii inatokana na makubaliano ya maridhiano yaliofikiwa karibuni baina ya Rais Amani Karume wa Visiwa vya Zanzibar na katibu mkuu wa chama cha CUF, Seif Shariff Hamad, katika kulituliza joto la mfarakano lilokuweko baina ya kambi mbili za kisiasa, CCM na CUF, huko Zanzibar.
Othman Miraji amezungumza na John Chiligati, katibu mwenezi wa chama cha CCM nchini Tanzania na ambaye pia ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi. Alizungumza hivi juu ya wazo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar...
0 comments