Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kamala awapa siku saba Wachina

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala ametoa siku saba kwa uongozi wa Kampuni ya Geo China Constraction (GCC) inayojenga barabara ya Arusha-Namanga kuondoa vifaa vichakavu na kuleta vipya ili kurekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye ujenzi huo.
Kamala alisema hayo juzi alipokuwa akikagua barabara hiyo ambayo ujenzi wake umekuwa ukisuasua kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
Alisema ujenzi huo umekuwa ukisuasua kutokana na kampuni hiyo kutumia vifaa ambavyo vinaonyesha kuchakaa na kwamba hawana utaratibu wa kuagiza vifaa vipya kwa wakati..
Waziri Kamala alisema mkataba unaonyesha matengenezo ya barabara hiyo yalitakiwa yawe yamefikia nusu ya kilometa 104, lakini hadi sasa ni asilimia 17 tu iliyokamilika.
Alisema kabla ya kuanza matengenezo, mkandarasi huwa anapewa fursa ya kuandaa vifaa ambavyo vinatakiwa kutumika kwenye ujenzi, lakini inaonekana kampuni hiyo haikufanya hivyo.
'”Kwa jinsi nilivyoona hapa hakuna vifaa muhimu vya ujenzi vinavyopaswa kuwepo… nimegundua mtambo wa kusambazia lami ni mbovu kitendo ambacho kwa ujenzi wa barabara ni hatari, jambo hili hatuwezi kulifumbia macho,” alisema.
Tags:

0 comments

Post a Comment