Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Pinda kujichanganya Krismas jimboni kwake.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Pinda kujichanganya Krismas jimboni kwake.

Kuanzia Desemba 22 ndani ya mwaka huu anatarajia kufanya ziara yake hadi hapo Januari 2 mwakani, huku akishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo wilayani Mpanda mkoani Rukwa. Si mwingine bali ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwani anatarajia kufnaya ziara yake jimboni kwake siku za usoni, na atakuwa mgeni rasmi ndani ya mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mpanda. Naye Afisa uhusiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Willy Sumia, alisema kwa njia ya simu kutoka Mpanda kwamba ndani ya Desemba 23 hadi 24...Waziri Mkuu atafanya ziara yake ya kutembelea wapiga kura wake katika tarafa ya Mpibwe Wilayani humo. Ndani ya Desemba 26 mwaka huu Waziri Mkuu atatembelea Hifadhi ya Wanyama ya Katavi ambako atakuwepo huko hadi Desemba 30 atakaporejea kijijini kwao Kibaoni. Mbali na hilo pia Desemba 31 mwaka huu, Waziri Mkuu atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya wa 2010, na kuuaga mwaka 2009 ambazo zitafanyika mjini Mpanda. Januari Mosi 2010, Waziri Mkuu atashiriki Ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Katoliki la Mpanda na siku inayofuata atakuwa Mjini Mpanda ili kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na Januari 3, atarejea Mbeya kwa ajili ya safari ya kurudi Dar es Salaam.

Tags:

0 comments

Post a Comment