Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Yanga ngangari Tusker

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

25.11.2008 0005 EAT

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema hautayumbishwa kuhusiana na msimamo wake wa kujitoa katika michuano ya Kombe la Tusker kama ratiba ya mashindano hayo itabaki kama ilivyo. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambayo ina mkataba wa kuidhamini Yanga pamoja na Simba, ambapo mkataba huo pamoja na mambo mengine kuna suala linalozungumzia timu hizo kushiriki mashindano yote yatakayoandaliwa na kampuni hiyo, huenda ikajitoa kuidhamini Yanga kama timu hiyo itaendelea na msimamo huo wa kujitoa. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema pamoja na kuwepo kipengele hicho, katika mkataba wao, lakini kutokana na kubanwa na ratiba itakuwa ngumu wao kushiriki. Alisema wataendelea na msimamo wao wa kutoshiriki michuano hiyo, hadi hapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), litakapobadili ratiba ya michuano hiyo, ambayo Yanga ni bingwa mtetezi. Alisema kutokana na ratiba ya timu ya Taifa kuingiliana na michuano hiyo, wachezaji wao hawatakuwa na muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu, badala yake watataka kutumia muda huo kufanya maandalizi yao hivyo itakuwa ngumu kushiriki michuano hiyo. "Moja kati ya masharti katika mkataba na TBL ni kushiriki michuano yao lakini kutokana na kubanwa na ratiba michuano hii watatusamehe hatuwezi kushiriki," alisisitiza Madega. Lakini alisema kwa vile TBL waliingia mkataba na klabu hizo mbili kwa kukaa mezani, hivyo haamini kama watakatisha mkataba wao kupitia vyombo vya habari na kwamba kama kutakuwa na suala hilo wangetoa taarifa rasmi. Yanga ilitangaza kujitoa katika michuano hiyo mwishoni mwa wiki kwa madai ina wachezaji wengi Taifa Stars, ambao watakaa na timu hiyo hadi Desemba 14, wakati Kombe la Tusker linaanza Desemba 15 mwaka huu, hivyo kuishauri TFF isogeze mbele michuano, kauli ambayo TFF imeikataa.

0 comments

Post a Comment