Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kortini kwa kulawiti msikitini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MHUDUMU wa msikiti wa Babati Mjini, Athumani Mdoe Sogora, 30, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa akiwa ndani ya nyumba hiyo ya ibada mkoani Manyara.

Tukio hilo la linadaiwa kutendwa na mtuhumiwa Novemba 6 mwaka huu majira ya saa 4:00 wakati Sogora alipomlawiti kijana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Bonga.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Parmena Sumary kwa niaba ya Kamanda Luther Mbutu, baada ya sala ya jioni, mtoto huyo alikuwa amelala msikitini.

Taarifa inaeleza kwamba mtoto huyo alilala msikitini baada ya kutoroka nyumbani kwao kijiji cha Bonga na ndipo saa 04:00 mhudumu huyo alimlawiti na mtuhumiwa amekamatwa na alifikishwa mahakamani Jumanne ya Novemba 11. Wakati huohuo, mkulima mmoja wa kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati ameuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo, Catherine Lohay, 40,) aliuwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Eliazeri Sosia, 64, kutokana na kutoelewana kwao kwa muda mrefu. Tayari mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara uchunguzi wa polisi utakapokamilika.

Katika tukio jingine lililotokea kwenye kijiji cha Galapo wilayani Babati, mkazi aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Agostino, 43, alipigwa kichwani na kijiko kikubwa cha kuchotea supu kwenye klabu ya pombe za kienyeji na kujeruhiwa vibaya kabla ya kufariki Novemba 10.

Inadaiwa kuwa Emmanuael alichota supu bila ya idhini kutokana na kuwa katika hali ya ulevi na hivyo kusababisha Pascal Batholomeo, 70, kuchukia na kumpiga kwa kijiko hicho kikubwa cha kuchotea supu. Mtuhumiwa amekamatwa na polisi.

Tags:

0 comments

Post a Comment