KITUO Cha Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mbalimbali hapa nchini (UNIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo wameandaa maadhimisho ya siku ya Michezo na Amani Duniani yatakayofanyika Septemba 21 katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo ambayo yamelenga kukuza uelewa wa ambavyo michezo inavyoweza kuvunja mipaka inayogawanya jamii ikiwa ni nyenzo yenye nguvu ya kuzuia migogoro na kusaidia juhudi za kukuza amani ikiwa ni pamoja na kuleta ushirikiano katika michezo kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mwakilishi wa UN, Harrieth Macha alisema kwa upande wa Tanzania mambo mbalimbali yameandaliwa katika kusherehekea siku hiyo ikiwemo maandamano kwa ajili ya kuenzi amani pamoja na michezo mbalimbali kuonyeshwa ambayo itajumuisha wanafunzi zaidi ya 2, 400 kutoka shule mbalimbali.
Alisema kutakua na onyesha maalum la kukuza uelewa na kuonyesha nini Mashirika ya Tanzania yanafanya juu ya Michezo na amani ambapo vikundi mbalimbali vya Wanamuziki maarufu Nchini wanaoelimisha jamii hususan vijana katika maswala ya maisha watatoa burudani.
Afisa Michezo kutoka Wizara ya Habari , Utamaduni na Michezo, Nicholous Bulamile alisema kwa upande wao wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo na wameandaa mambo mbalimbali yatakayoenzi siku ya amani na Michezo lengo likiwa ni kuendeleza michezo ndani na nje ya nchi.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni "Michezo ni nyenzo muhimu katika kudumisha Amani,Sote tudumishe amani kwa kuunganisha nguvu dhidi ya migogoro,umaskini na njaa na kuhakikishaheshima na haki kwa wote".
0 comments