Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - WAUSLAMU KUMUONDOA MUFTI WAO Shekhe Issa bin Shabaan Simba

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter BARAZA la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) limewataka Waislamu jijini Dar es Salaam kutojihusisha na vurugu za kumwondoa madarakani Mufti wa Tanzania, Shekhe Issa bin Shabaan Simba, zilizopangwa kufanyika leo kwani kiongozi huyo amewekwa kisheria Akizungumza Dar es Salaam jana, Mhadhiri Mkuu wa Baraza hilo, Shekhe Said Mwaipopo, alisema vipeperushi vimesambazwa kuhamasisha Waislamu leo kusali makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni na baada ya swala, wauondoshe madarakani uongozi halali wa Mufti Simba. "Nawaomba Waislamu wenzangu msijihusishe katika vurugu zozote, kwani huu ni Mwezi wa Toba, ambao kila Mwislamu anatakiwa kufanya toba," alisisitiza. Alisema mbinu hizo zinapangwa na viongozi waliofukuzwa BAKWATA wanaotaka kurudi kwa maslahi yao. Alitahadharisha, kwamba madhambi yao yataanikwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria karibuni. Shekhe Mwaipopo, alisema mgogoro unaoendelea wa nyama na tende zilizokwama bandarini, uliibuka wakati viongozi hao wakiwa madarakani na wakati huo Mufti Simba alikuwa India kwa matibabu, hivyo hahusiki kwa namna yoyote na jambo hilo. "Viongozi hao wanapodai tende zimeuzwa ni nani aliyeuza kama si wao, kwa sababu ndio waliokuwa makao makuu na kuratibu mambo yote ya Baraza. Tunaomba Waislamu wasitumiwe kama mishumaa," alishauri Shekhe Mwaipopo na kuongeza kuwa Uislamu una taratibu zake na kama kuna matatizo, watakaa na kurekebishana. Walioandaa mapinduzi hayo ni Kamati Maalumu ya Vijana wa Kiislamu Dar es Salaam, kwa nia ya kuwarudisha madatrakani mashekhe na maulamaa waliofukuzwa na 'kudhalilishwa' kinyume na Katiba ya Baraza. Hivi karibuni baadhi ya viongozi waandamizi wa BAKWATA walitimuliwa kwa tuhuma mbalimbali yakiwamo madai ya kuandika mikataba batili na kufuja mali za Waislamu.
Tags:

0 comments

Post a Comment