Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Makubaliano ya Zimbabwe yafichuliwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Taarifa zilizofichuliwa katika makubaliano ya kugawana madaraka yaliyofikiwa siku ya Alhamisi zimesema kuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, anatarajiwa kuendelea kudhibiti jeshi na kuwa msimamizi wa vikao vya bunge.

Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amesema Bw Mugabe amekubali kugawana madaraka na Bw Morgan Tsvangirai lakini taarifa zaidi zitatolewa siku ya Jumatatu.

Taarifa hizo pia zimesema Bw Tsvangirai atadhibiti jeshi la polisi na kusimamia baraza jipya la mawaziri.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kuwepo na mazungumzo yaliyodumu kwa wiki saba kufuatia uchaguzi wa mwaka huu nchini humo uliogubikwa na ghasia.

Bw Mugabe bado hajatoa kauli yeyote kuhusiana na makubaliano hayo yaliyosimamiwa na kiongozi wa Afrika Kusini.

Taarifa zote kutoka shirika la utangazaji la BBC zimezuiliwa nchini humo.

Hata hivyo, mwandshi wa BBC aliyopo Zimbabwe amesema wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC hawajaonekana mitaani wakisherehekea muafaka huo.

Na wakati huo huo, wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF hawajaonekana kupinga makubaliano hayo.

Tags:

0 comments

Post a Comment