MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila ambaye anatoa tiba ya magonjwa sugu amesema kuwa kuna kasi kubwa ya wagonjwa mahututi wanaletwa kwake kutoka Kenya, hivyo akaiomba Serikali ya Tanzania iingilie kati ili kuwazuia.
Akizungumza jana kijijini hapa, Mwasapila alisema amepewa taarifa kuwa wagonjwa wanaopelekwa kwake kutoka huko wanatolewa hospitali. Alisema si vyema kupelekewa wagonjwa mahututi kwa sababu hakuna miundombinu mizuri pamoja na huduma hali inayohatarisha maisha yao.
"Kutokana na wagonjwa mahututi huletwa hapa Samunge imekuwa inasababisha wagonjwa wengine kufariki bila ya kupata tiba," alisema Mwasapila Mwandishi jana alishuhudia gari la wagonjwa (ambulance) lenye namba za usajili za Kenya likielezewa kuwa limetokea Nairobi likiwapeleka wagonjwa kwa mchungaji huyo maarufu kwa jina la Babu.
Kwa sababu hiyo, Babu ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha na barabara ya kwenda kijijini huko ni mbaya.
Tiba ya Babu kujadiliwa na Bunge la EAC
Mbunge wa Afrika Mashariki (Kenya), Lubeni Oyondi jana alifika Samunge kupata kikombe na kuahidi kufikisha changamoto kwa upatikanaji wa tiba hiyo kwenye Bunge hilo.
Tiba ya Babu kujadiliwa na Bunge la EAC
Mbunge wa Afrika Mashariki (Kenya), Lubeni Oyondi jana alifika Samunge kupata kikombe na kuahidi kufikisha changamoto kwa upatikanaji wa tiba hiyo kwenye Bunge hilo.
Oyondi alisema kutokana na maelfu ya watu wa Afrika Mashariki na nje kufika hapa, ni lazima barabara inayoelekea Samunge ipewe hadhi inayostahili.
"Nimefika hapa Samunge nimejionea hali ya barabara mbaya, nadhani nitalifikisha suala hili kwenye kikao kijacho cha Bunge ili tuone tutawezaje kusaidia miundombinu ya eneo hili,’’ alisema Oyondi.
Alisema eneo hilo la Samunge linaweza kutumika kutangaza sehemu ya utalii na hivyo kuongeza kipato katika nchi za Afrika Mashariki’.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi ilishindwa kukabidhi vitabu vya ushuru wa magari na helikopta kwa viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Samunge
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Maiko lengume alisema wamepewa ahadi ya kukabidhiwa vitabu hivyo baada ya kupatiwa semina ambayo itajumuisha wajumbe 25 wa serikali ya kijiji, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukusanya mapato.
0 comments