IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Jerusalem:
Israel imesema itaizuwia meli ya misaada kutoka Libya ,kuelekea katika Ukanda wa Gaza. Meli hiyo iliondoka jana kutoka bandari moja ya Ugiriki. Licha ya juhudi za kibalozi kuitaka meli hiyo ielekee Misri, Israel imesema inaelekea iko njiani kwenda Gaza. Waziri mmoja wa Israel alisema kuziruhusu meli kufika Gaza bila ya kukaguliwa kutakuwa na athari kubwa kwa usalama wa Israel. Waziri wa ulinzi Ehud Barak amesema juhudi za Libya kukiuka hatua ya Israel ya kuufunga Ukanda wa Gaza unaotawaliwa na chama cha Hamas, ni "uchokozi usiohitajika."
You Are Here: Home - - Israel yasema itaizuwia meli ya misaada ya Libya kwenda Gaza
0 comments