Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Hivi kweli ni haki kwa nyumba mbili za kuishi familia mbili kujengwa kwa Tsh. 2.5 bilion hela ya walipa kodi wa Kiafrica?

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KAMATI YA ZITTO KUMWEKA KITIMOTO GAVANA WA BOT

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imepanga keshokutwa kuwa siku ya kumwita gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ajieleze kuhusu matumizi ya Sh 2.5bilioni kujenga nyumba mbili za kuishi...
Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa POAC, Ester Kilasi zimeeleza kuwa Profesa Ndulu ataitwa katika kamati hiyo baada ya wajumbe wake kufanya ziara eneo la mradi kulikojengwa nyumba hizo.

Kilasi aliliambia gazeti hili jana kuwa ziara hiyo itafanyika kwa siku mbili; leo na kesho.

"POAC imemwita Profesa Ndulu Alhamisi hii (kesho kutwa) ili atupe maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba anayoishi na za manaibu gavana wake," alisema Kilasi na kuongeza:

"Lakini kabla ya kupata maelezo hayo kamati imeamua kufanya ziara ya kuzungukia na kuangalia hali halisi ya mradi wa ujenzi wa nyumba hizo tujiridhishe." alisema.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kwamba Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe ambaye yuko masomoni Ujerumani amelazimika kurudi nchini kusimamia sakata hilo.

Kamati hiyo itakutana na Profesa Ndulu siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo.

Mkulo aliliambia gazeti hili Ijumaa iliyopita kuwa ripoti ya kamati hiyo imekwishawasilishwa kwake na yeye ameanza kuipitia kabla ya kuitoa hadharani.

"Nikitoka hapa ninakwenda kuisoma ripoti niliyoiagiza kuhusu matumizi ya fedha yaliyotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya gavana na manaibu gavana," alisema Mkulo na kuongeza:

"Hizi tuhuma ni nzito na zinamhusu mtu nyeti wa serikali, hivyo itachukua muda kidogo kutoa majibu ya ripoti niliyonayo."

Mkulo alifafanua kuwa amechelewa kuitoa ripoti hiyo kutokana na kuhusika kwa vyombo vingine nyeti vya serikali katika uchunguzi wake.

"Nikimaliza kuisoma ripoti hii, nitalazimika nishauriane na washauri wangu na kisha nivishirikishe vyombo vingine nyeti vya serikali," alisema

Kwa mara ya kwanza taarifa ya matumizi ya fedha katika ujenzi wa nyumba hizo ziliripotiwa na gazeti hili, lakini baadaye BoT ilitoa ufafanuzi ikieleza kuwa nyumba hizo zilijengwa baada ya kufuatwa taratibu zote za zabuni.

Kabla BoT kujibu tuhuma hizo, Profesa Ndulu alikiri kutumika kwa kiasi hicho cha fedha, lakini akafafanua kuwa fedha ilitumika kujenga upya nyumba hizo na siyo kuzikarabati.

"Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu, ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema," alilalamika gavana huyo.

CHANZO: MWANANCHI
Tags:

0 comments

Post a Comment