Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - JK ataka wapangaji walioathiriwa na mafuriko kufikiriwa viwanja

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka Kamati ya Maafa inayoshughulikia waathirika wa mafuriko yaliyoikumba Dar es Salaam mwaka jana, kufikiria namna ya kuwapatia viwanja waliokuwa wapangaji kwenye nyumba zote zilizobomelewa kwa mafuriko.


Pamoja na kutoa agizo hilo, pia ameitaka kamati hiyo kuwa makini katika ugawaji wa viwanja hivyo.


“Msipokuwa makini zoezi hili haliishi… mtaendelea kufanya hivi kila siku watajitokeza pia wasiostahili watakuja kudai viwanja,” alisema Rais Kikwete muda mfupi kabla ya kukabidhiwa na kukagua mahema hayo.


Rais alisema hayo wakati wa kupokea bidhaa mbalimbali zilizotolewa na Kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) kwa ajili ya waliokumbwa na mafuriko.


Kampuni hiyo pamoja na kutoa vifaa hivyo, pia imeahidi kujenga kituo cha polisi, vyumba 14 vya madarasa, ofisi za walimu na chumba cha kulia chakula kwa ajili ya waathirika wa
mafuriko watakaohamia Mabwepande nje ya jiji la Dar es Salaam.


Mbali na ahadi hiyo, HSC imetoa mifuko 2,000 ya saruji, vyombo vya ndani na taa za sola kwa familia zote 653 zitakazopatiwa makazi kwenye eneo hilo.


Mkurugenzi wa HSC, Gharib Said Mohamed alisema hayo katika hafla ya Kamati ya maafa mkoani hapa kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete mahema 203 yaliyojengwa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS).


Gharib amesema kwamba shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi na jengo la kulia
chakula vitakamilika katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.


“Kwa kweli mpaka sasa kwenye saruji, vyombo vya ndani na taa za sola tumetumia zaidi ya Sh milioni 70, kuhusu ahadi ya ujenzi wa kituo cha polisi na shule mpaka sasa gharama yake hatujaijua hadi vitakapokamilika,” alisema Gharib.

0 comments

Post a Comment