IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Robo fainali ya michuano ya 35 ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge inaanza leo (Desemba 5) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi ya kwanza itakayochezwa saa 8.00 mchana itazikutanisha Burundi na Sudan wakati ya pili itakayoanza saa 10.00 jioni itakuwa kati ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) dhidi ya Rwanda.
Kesho (Desemba 6) mechi ya kwanza ya robo fainali itakuwa kati ya Uganda na Zimbabwe wakati ya pili itakayoanza saa 10.00 jioni itawakutanisha mabingwa watetezi Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na Malawi (The Flames). Mechi zote zitaoneshwa moja kwa moja kupitia SuperSport 9.
Viingilio kwa mechi zote za robo fainali ni sh. 2,000 kwa viti vya kijani na bluu, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 kwa VIP A.
You Are Here: Home - HABARI ZA LEO , HABARI ZA MICHEZO - Robo fainali ya kombe la CECAFA kuanza leo
0 comments