Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Hali ya Usalama Ivory Coast inatia wasiwasi. Ouattara aamuru jeshi kurudi kambini

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anaendesha harakati kali kudhibiti nidhamu ya jeshi.
Amewapa saa 48 askari wa jeshi jipya la nchi hiyo FRCI, kurudi kwenye kambi zao.


Jeshi hilo lina wapiganaji waasi wa zamani.
Inafuatia ghasia kutokea mwishoni mwa wiki katika mji wa magharibi wa Vavoua ambako askari wasio watiifu waliwaua vijana sita.
Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa Jumatatu kati ya Bw Ouattara na washauri wake wa juu wa kijeshi.
Doria za kijeshi zimepewa saa 48 kufungwa. Rais Ouattara alitamka kutovumilia vitendo vyovyote vya ghasia.
Mwandishi nchini humo Selay Kouassi anasema kuwaamuru askari warudi kambini ni hatua ya kwanza kuelekea kufanyika kwa sensa kujua nani ni askari na nani si askari.
Anasema wapiganaji waliomsaidia Bw Ouattara kumwondoa mtangulizi wake Laurent Gbagbo, si miongoni mwa wanajeshi rasmi na hawajaweka silaha chini.
Watu wapatao 3,000 waliuawa katika mapigano kufuatia uchaguzi wa Novemba 2011 kabla ya Bw Gbagbo kukamatwa na vikosi vilivyomuunga mkono Ouattara vikisaidiwa na Umoja wa Mataifa na Ufaransa mwezi April.
Rais wa zamani anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mahakama ya ICC alikopelekwa mwezi uliopita.
Anatuhumiwa ‘kuhusika’ na mauaji, ubakaji, utesaji na vitendo vingine kinyume na utu baada ya kukataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi.
Bw Gbagbo anakuwa ni mkuu wa nchi wa kwanza kukabiliwa na kesi ICC.

0 comments

Post a Comment