IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
*Wafanyakazi wagoma kudai nyongeza ya malipo
MELI nne zikiwemo za Mashirika ya Misaada ya Kimataifa kutoka mataifa mbalimbali Duniani zilizosheheni mizigo zimekwama kwa siku ya tatu sasa katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na vibarua wa kushusha mizigo bandarini hapo kugoma.
Washusha mizigo hao wamegoma kudai nyongeza ya malipo ya kazi zao ambao ni sh. 5,000 kwa siku kiwango wanachoeleza kuwa ni kidogo kilinganishwa na kazi wanayofanya na kuporomoka kwa thamani ya shingili ambako kumefanya kuwe na ugumu wa maisha.
Vibarua hao walionekana wakiwa wamejikusanya makundi makundi nje ya majengo katika ofisi za madalali wa makampuni yaliyopewa zabuni ya kushusha mizigo bandarini hapo huku wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wanaotoka nchi za nje wakiwa wanailalamikia serikali kutomaliza tatizo hilo.
Wakizungumza na gazeti hili jana, baadhi ya vibarua hao walisema mgomo huo ulioanza Desemba 4, utaendelea hadi hapo watakaporekebishiwa kiwango cha malipo kama wanavyodai kwa kuwa wamevumilia muda mrefu wakifuata taratibu zote bila mafanikio.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, mfanyakazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Ally Wandu, alisema wanataka kulipwa sh.150 kwa kila mfuko wa kilo 50 unaoshushwa tofauti na sasa ambapo wanalipwa sh. 30.
Alisema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumuna hatari huku wakilipwa sh. 30 kwa mfuko wa kilo 50 na kwamba kiwango hicho ni kidogo mno na hakiwezi kukidhi mahitaji yao hasa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Bw. Wandu alisema wanapofuatilia madai yao kwa viongozi wa makampuni hayo yaliyopewa kazi ya kushusha mizigo bandarini wanaelezwa kuwa hiyo ndiyo bei waliopangiwa na Mamlaka ya Bandari hivyo hawawezi kuongeza kiwango hicho cha fedha.
"Kila tukifuatilia kwa viongozi wa hayo makampuni ya udalali hudai kuwa kiwango cha sh. 30 kimeamriwa na bandari hivyo hawawezi kuongeza na kwa wale wanaotaka kazi wafanye na wasiotaka waondoke," alisema.
Alisema walipofuatilia zaidi kwa viongozi hao waliambiwa kwamba wanaongeza sh.10 kwenye sh.30 ya awali kiwango ambacho bado hakiwezi kuwasaidia chochote hivyo wakaamua kuingia katika mgomo usio na kikomo hadi watakaposikilizwa.
Walisema kuwa kutokana na mgomo huu ulioanza juzi walionana na baadhi ya maofisa wa bandari na kuelezwa kwamba wasubiri hadi Januari mwakani Mkurugenzi Mkuu wa Bandari atakaporudi kutoka nchini China.
Walisema mbali na kiwango kidogo cha ujira wanacholipwa pia wamekuwa wakifanyakazi katika mazingira magumu na hatarishi kutokana na kutokuwepo kwa vyoo na maji katika maeneo waliyotengewa.
"Tunataka kuanzisha umoja wetu ambao utaingia mkataba kwa kuwa tumechoka kuonewa na kudhulumiwa haki zetu, umefika wakati sasa kampuni hizo tano ziondolewe," alisema mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Paulo.
Mwandishi wa habari hizi alipofika Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kupata ufafanuzi kuhusu madai hayo ya wafanyakazi, mmoja wa ofisa aliyeomba jina lake kutotajwa kwa madai kuwa si msemaji alisema yeye si msemaji hawahusiki na suala hilo.
"Kuna makampuni ambayo yamepewa kazi hiyo, ili kupata ukweli wa hilo fuatilia kwa viongozi wa makampuni hayo," alisema ofisa huyo.
Hata hivyo mwandishi alipofuatilia kwenye ofisi za makampuni hayo nyingi zilikuwa zimefungwa huku chache zilizokuwa wazi alijibiwa kuwa
You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Balaa tena Bandari ya Dar es Salaam
0 comments