Siku nne za machafuko na maandamano katika uwanja wa Tahrir na maeneo mengine kadhaa zimeuweka utawala wa kijeshi kwenye wakati mgumu, huku waandamanaji wakidai kuwa viongozi wa mpito chini ya Baraza la Kijeshi hawana dhamira ya kupisha serikali ya kidemokrasia.
Baraza la Mawaziri lilijiuzulu hapo jana, na sasa jeshi limesema kuwa nafasi yake itachukuliwa na kile ilichokiita "baraza la uokovu la kitaifa" hadi mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Wakati huo huo, idadi ya watu waliouawa tangu kuanza kwa maandamano yaliyoanza juzi dhidi ya utawala wa kijeshi imefikia 34, baada ya mtu mwengine kuuawa alfajiri ya leo. Madaktari wanasema vifo vingi vinatokana na mabomu ya machozi, huku saba kati yake vikithibitishwa kusababishwa na risasi.



0 comments