Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KISIASA , HABARI ZA LEO - Rais Kikwete akubali kukutana na Chadema

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuomba viongozi wa chama hicho kukutana na Mheshimiwa Rais kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mheshimiwa Rais Kikwete amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu ni jambo jema.

Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Mheshimiwa Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa CHADEMA na kuzungumzia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 22, 2011
DODOMA

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILIVYOENDELEA JANA MJINI DODOMA

0 comments

Post a Comment