Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Urusi yapinga vikwazo vipya dhidi ya Iran

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Urusi imesema vikwazo vipya dhidi ya Iran havikubaliki, ikiwa ni siku moja baada ya Marekani kutangaza hatua zaidi, dhidi ya utawala wa Iran. Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, imetoa taarifa leo ikisema vikwazo hivyo vinakiuka sheria za kimataifa. Jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema vikwazo vipya vya nchi yake vinaelekezwa kwenye sekta ya mafuta na gesi ya Iran. Wakati huo huo, Shirika la Nguvu za Atomiki la Umoja wa Mataifa limesema lina kila sababu ya kuamini kuwa Iran inajaribu kutengeneza vichwa vya makombora ya nyuklia. Serikali ya Iran inapinga kwa kusema kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya kuzalishia nishati tu.

0 comments

Post a Comment