Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Je, Papa Benedict wa 16 ameonesha ishara ya Freemanson

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Papa Benedict XVI.
Hamida Hassan na Mitandao
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Joseph Aloisius Ratzinger ‘Papa Benedict XVI’, ameushtua ulimwengu, ishara ya vidole na mikono wakati wa kutoa salamu katika picha zilizotundikwa mitandaoni, vimefananishwa na alama za Jamii ya Siri (Secret Society) inayoitwa Freemasons.

Tony Blair akisalimiana na Papa.
 
Zipo taarifa kuwa Freemasons kwa sehemu kubwa wanamuabudu Shetani (Jini Mkuu) anayeitwa Lucifer ndiyo maana imekuwa ikiitwa Dini ya Shetani.

Wachambuzi wa mambo ya Freemasons wanaeleza kuwa jamii hiyo ya siri inapiga vita Uislam na Ukristo hali ambayo imeibua mshtuko baada ya picha hizo kumuonesha Papa Benedict akitumia alama za watu ambao ni maadui wa madhehebu anayoyaongoza.

Picha zilizoibua maswali na mshtuko, moja inamuonesha Papa akiwa anatoa salamu ya vidole ambavyo amevitengeneza kama pembe ya mbuzi, nyingine akiwa anapeana mikono na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair.

Inadaiwa kuwa mtindo wa kupeana mikono walioutumia Blair na Papa, si wa kawaida, kwani mara nyingi hutumiwa na memba wa Freemasons wanaposalimiana au kupongezana.

Barack Obama.

MASWALI TATA
Kutokana na picha hizo za Papa, imeibuka mijadala mingi mitandaoni kuhusu imani ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki lakini mwisho kumekuwa na maswali matano ambayo yamekosa majibu:

MOSI: Papa Benedict ni Freemason?
PILI: Ni mfuasi wa jamii inayopingana na maono ya kanisa analoongoza?

TATU: Kama siyo Freemason, je, anawakubali na kuwasapoti?
NNE: Je, alitoa salamu bila kujua maana yake?
TANO: Papa alitumia salamu hiyo kumkejeli Shetani ambaye ndiye mkuu wa Freemasons?

http://www.jesus-is-savior.com/False%20Religions/Wicca%20&%20Witchcraft/bush_satan_sign.jpg
George W. Bush.

WAKATOLIKI WALAANI
Kwa mujibu wa maelezo ya watu ambao wamejipambanua kwamba ni waumini wa madhehebu ya Kanisa Katoliki, picha hizo zenye ishara ya vidole vya ki-Freemasons, zimetengenezwa kwa lengo la kuwafanya Wakatoliki watilie shaka mwenendo wa kiongozi wao.

Rahel Ratzega aliyejitambulisha kuwa ni Mkatoliki, raia wa Sweden alisema wakati anachangia habari ya Papa na vidole vya ki-Freemasons: “Mimi ni mtaalamu wa kompyuta, picha ya Papa imewekewa vidole vya mfuasi wa Freemasons ili kutuchafua Wakotiliki.

http://files.myopera.com/philiconvallley/albums/8711752/thumbs/hillary%20clinton%20freemasons.jpg_thumb.jpg
Hillary Clinton.
 
“Mimi na Wakatoliki wenzagu wa kanisa letu la Nytorv Square tumelaani hili, tumeujua ukweli kwamba picha ya Papa imetengenezwa. Tunaamini Freemasons ndiyo waliotengeneza ili kuwafanya Wakatoliki waone kiongozi wao ni mfuasi wa imani zenye mrengo wa Shetani.

“Tunamuamini Mungu, Shetani hayupo na sisi. Freemasons ni maadui wa Wakatoliki.”
Kuhusu picha ya Papa kushikana mikono na Blair, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alitegwa.

Margaret Ryan, aliyejitambulisha kuwa ni Mkatoliki anayesali kanisa lililopo Newington, London, England, alisema: “Tunamtambua Blair ni Freemason, kwa hiyo alichokifanya ni kumtegea mkono Papa.

Sarkozy na Gaddafi wakisalimiana kwa ishara za Freemason.

“Papa siyo Freemason, Blair alimfanyia usanii Papa, akampa mkono kwa mtindo wa Freemason, bila kujua Papa naye akakubali mkono wake kumbe kwa mwenzake hiyo ina maana kubwa.

“Blair ni mmoja wa waumini wa Freemasons wenye digrii za juu kabisa, hata ule mtego wake kwa Papa haukuwa wa hivi hivi, lengo lake lilikuwa ni kuukejeli Ukatoliki kwa sababu Blair mbali na Freemason pia anaabudu Anglikana.”

Hata hivyo, wamiliki wa mtandao uliochapisha picha hizo walisisitiza kuwa ni halisi na hazifanyiwa utundu wowote wa kikompyuta.
Bill Clinton.
 
FREEMASONS INAZIDI KUPATA UMAARUFU
Hivi karibuni Freemasons imekuwa ikipata umaarufu mkubwa huku watu wakifurika huko na wasiojua chochote juu ya dini hiyo wameendelea kusaka kuijua kiundani.

0 comments

Post a Comment