Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Hali si shwari. Israel yawaua wanausalama wa Misri

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Afisa mmoja wa jeshi la Misri na wanausalama wawili wameuawa katika shambulio lililofanywa na Israel dhidi ya wapiganaji, katika mpaka wa nchi hizo mbili hapo jana. Watu hao watatu waliuawa wakati wanajeshi wa Israel walipokuwa wakiwafurumusha wapiganaji katika mji wa kitalii wa Taba uliopo katika mwambao wa bahari ya Sham kusini mwa Sinai, ambao unapakana na mji wa Israel wa Eilat.

Mapema jana watu waliokuwa na silaha waliwaua watu saba, kusini mwa Israel katika shambulio lililofanywa mpakani mwa Misri, hali iliyosababisha majeshi ya Israel kuushambulia Ukanda wa Gaza na kuwaua Wapalestina sita, akiwemo mtoto. Israel imekuwa ikiilaumu Hamas kwa tukio hilo, lakini serikali ya Hamas ambayo inaudhibiti ukanda wa Gaza imekanusha kuhusika katika mashambulio hayo.

0 comments

Post a Comment