IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Kuna taarifa kuwa mbu wameanza sugu haraka kwa vyandarua vilivyotiwa dawa, utafiti uliofanyika nchini Senegal umeonyesha.
Katika miaka ya karibuni matumizi ya vyandarua vyenye dawa yamekuwa ndio njia kuu ya kuzuia malaria hasa barani Afrika.
Kwa mujibu wa Jarida la Utafiti wa Kisayansi kwa magonjwa ya kuambukiza la Lancet, watafiti hao pia wanasema vyandarua hivyo vinapunguza uwezo wa kuhimili maradhi ya malaria kwa watoto wakubwa na watu wazima.
Lakini waatalam wengine wanasema utafiti huo ulikuwa mdogo kufikia maamuzi kuhusu uwezo wa vyandarua kwa muda mrefu.
Katika vita dhidi ya malaria silaha rahisi na yenye uwezo mkubwa moaka sasa imekuwa vyandarua vilivyotiwa dawa yamuda mrefu.
Katika miaka michache iliyopita vyandarua vimekuwa vikisambazwa barani Afrika na kwingineko –na Shirika la Afya Duniani –WHO linasema kama vikitumika vizuri vinaweza kupunguza nusu ya athari zinazotokana na malaria.
Iwapo huu ndio mwenendo tunaoushuhudia katika sehemu za Senegal basi ina umuhimu kwa siku zijazo katika mikakati ya kudhibiti na kuzuia malaria. Alisema Dr. Joseph Keating wa Chuo kikuu cha Tulane
Nchini Senegal, vyandarua vyenye dawa milioni sita vimesambazwa katika miaka mitano iliyopita. Katika utafiti huo uliofanyika katika kijiji kidogo nchini humo na kufuatilia matukio ya malaria kabla na baada ya kuanza kusambazwa kwa vyandarua hivyo mwaka 2008.
Katika kipindi cha wiki tatu tangu kuanza kutumika, wanasayansi walikuta kuwa maambukizi yalianza kushuka –matukio ya ugonjwa huo yalikuwa chini ya mara 13 kabla vyandarua havijaanza kutumiwa.
Watafiti pia walichukua sampuli za Anopheles gambiae, mbu mwenye kusambaza vilemelea vya malaria kwa watu Afrika. Kati ya mwaka 2007 na 2010 uwiano wa vijidudu vilivyokuwa sugu kwa aina moja ya dawa vilipanda kutoka 8% hadi 48%.
You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mbu waonyesha usugu vyandarua vyenye dawa
0 comments