Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mume, Mke wachomana visu guest

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Habari kwa hisani ya Global Publishers

Mume Lucas John Komba (26), akiwa hoi na kisu alichojichoma tumboni mara baada ya tukio, bado yuko hai! Hadi leo, mume hajapata fahamu na yungali hospitali ya Muhimbili chini ya ulinzi wa Polisi.


Na Rhobi Chacha
SIYO filamu wala igizo, bali ni tukio la kweli lililozua hekaheka katika Kitongoji cha Shekilango, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea Juni 6, mwaka huu saa 11:00 za jioni ambapo mke na mume walikimbizana wakitokea katika Nyumba ya Wageni ya A Plus Lodge, chumba namba 3 huku wakiwa watupu, Gazeti la Amani linakudadavulia kisa kizima.

Wakiwa wanakimbizana, mwanamke akiwa mbele alionekana kushikilia tumbo huku utumbo ukining’inia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu na mwanaume huyo.

Mwanamke huyo aliyekuwa akipigania kuinusuru roho yake alikuwa akitoa maneno ya kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema akisema: “ Jamani nisaidieni, mume wangu anataka kuniua, anasema nimemsaliti.”



Marehemu Happy akiwa kwenye gari la polisi akipelekwa mochwari


Hata hivyo, mwanamke huyo hakuweza kufika mbali kwani alianguka chini na baada ya sekunde chache akatokea mume wake, naye akiwa mtupu huku kisu kikiwa kinamning’inia tumboni baada ya kudaiwa kuwa alijichoma.

Haikuchukua muda mrefu umati wa watu ukafika eneo hilo na kupigwa na bumbuwazi juu ya tukio zima, huku wengine wakisema watu hao walikuwa wamefumaniana.





Muda mfupi baadaye askari wa jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuwachukua watu hao, wakawapeleka katika Kituo cha Polisi cha Urafiki na kufungua jalada la kesi namba URP/ RB/ 5126/2011 Mauaji.


Baada ya kumaliza taratibu za kipolisi ndipo watu hao walipopelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na baadaye zikapatikana taarifa kuwa, mwanamke huyo alifariki dunia pale pale huku mwanaume akiendelea kuvuta hewa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanalifuatilia na pia alithibitisha kifo cha mwanamke aliyemtaja kwa jina la Happy Samweli au Nyaso anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 27-30.


Hata hivyo, Wambura alisema kwa mujibu wa kitambulisho cha kupigia kura kilichokutwa eneo la tukio, mwanaume huyo ametambulika kwa jina la Lucas John Komba (26), mwenyeji wa Songea, Ruvuma lakini alikuwa amejiandikisha Kiabakari, Kata ya Ukilango, Nyamiskye mkoani Mara.
Polisi imegundua kuwa mke na mume hao waliingia katika nyumba hiyo Juni 5, mwaka huu asubuhi na mwanaume alijiandikisha kwenye daftari la mapokezi kwenye nyumba hiyo ya wageni kwa jina la Abdallah, mkazi wa Tabora.

“Polisi walipofika eneo la tukio na kuingia ndani ya nyumba hiyo ya wageni walizikuta nguo za mwanaume na walipozisachi walikuta barua yenye ujumbe ulioandikwa na mwanaume,” alisema Wambura.



Kwa mujibu wa Wambura, barua hiyo ilikuwa ikimlalamikia mwanamke huyo, Nyaso kuwa amemwambukiza ugonjwa wa Ukimwi na amegundua hilo baada ya kwenda kupima.

Barua hiyo ya Komba iliendelea kudai kuwa, hatua hiyo aliyoichukua ni kwa sababu anaona amepotezewa dira ya maisha na mwanamke huyo.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Komba bado alikuwa haongei na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

0 comments

Post a Comment